MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, October 15, 2012

Waislamu Washambulia Makanisa Dar, Wachoma na Kuharibu Magari

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema mtoto mmoja (mkristu jina tunalo) akiwa katika michezo na mwenzake wa Kiislamu walianza kubishana, kuwa endapo ukikojolea kitabu cha dini ya Kiislamu (msaafu) lazima ugeuke kuwa kichaa, hivyo Josephat alibisha na kumwambia mwenzake anaweza kufanya hivyo na kutodhurika.

Baada ya mabishano hayo Josephat aliamua kukikojolea kile kitabu ili aone kama angelidhurika kama alivyoelezwa na mwenzake, lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo baadaye yule wa kiislamu alitoa taarifa kwa wazazi wake ndipo yalianza mazungumzo kati ya wazazi kwa wazazi.

Kova alisema mvutano huo ulifika katika kituo kidogo cha polisi na ndipo baadhi ya Waislamu walianza kujitokeza na kutaka wapewe maelezo na kadri ya walivyoongezeka eneo la kituo hali ilianza kuwa mbaya kwani baadhi yao walionekana kutaka kufanya fujo na kuomba wapewe yule mtoto ili wamuadhibu.
Baada ya hali kuwa tete Jeshi la Polisi lilileta askari wa kutuliza ghasia FFU kuwataka waliokuwa kituoni kuondoka kwa amani lakini baadhi yao walipinga hivyo kuanza kutumia nguvu kuwatawanya. “Baada ya wananchi hao kutawanyishwa baadhi walijikusanya na kuzunguka huku wakifanya fujo kwa kushambulia Makanisa, Makanisa yalioshambuliwa ambayo yote ni ya maeneo ya Mbagala Kizuiani ni pamoja na Kanisa la Anglikana, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT-Mbagala) na Kanisa la Sabato ambayo yamevunjwa vioo pamoja na kuharibu mali kama magari yaliyokuwa yameegeshwa eneo la kanisa na mengine waliokutana nao waandamanaji hao.na mali za watu,” alisema Kova akizungumza na chombo kimoja cha habari.
K.K.K.T Mbagala ambalo ndilo lilioharibiwa

Mlango wa kanisa ukiwa umevunjwa vioo

Akina mama wenye mzigo wa maombi, wakiomba Mungu awarehemu waliofanya uharibifu huo

Vyombo mbalimbali vya kanisa hilo vilivyochomwa moto

Watu mbalimbali waliofika kanisani hapo kujionea uharibifu uliotokea

Gari la Mchungaji wa usharika hou wa Mbagala likiwa limeharibiwa vibaya

Jionee uharibifu uliofanywa


Kushoto unaonekana msikiti walipotokea waumini wa dini ya kiislamu kwenda kufanya uharibifu huo.

Dean Geoge Fupe msaidizi wa Askofu mkuu wa kanisa la K.K.K.T Alipofika kanisani hapo kuona kulichojiri

Viti vikiwa vimerushwa huku na kule

Mimbari ya kuhubiria inavyoonekana baada ya kuchomwa moto

Mlango wa kanisa hilo na vitu mbalimbali vikiwa katika hali ya kusikitisha

Ofisi ya Mchungaji ilionekana hivi baada ya kutiwa moto

Inasikitisha sana

Mchungaji George Fupe akizungumza na mchungaji wa Mbagala juu ya yaliyojiri

No comments:

Post a Comment