MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, December 30, 2013

CVC WAFANYA SILVER JUBILEE

AIC Chang'ombe Vijana Choir jana wamefanya sherehe kubwa ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya hiyo. Sherehe hizo zilifanyika kanisani kwao eneo la Chang'ombe Sokota. Katika ibada iliyosheheni kwaya nyingi ikiwemo kwaya ya AIC Shinyanga, AIC Dar es Salaam Choir, Neema Gospel Choir (AIC), Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Kwaya ya Unjilisti Mtoni (Lulu), Kwaya ya Ukombozi toka K.K.K.T Msasani. Katika kuadhimisha miaka 25 ya kwaya hiyo pia walizindua jina jipya la kwaya yao na kuwa AICT Chang'ombe Choir na CVC kubaki kuwa Brand Name. 

 Watumishi wa Mungu walikuwepo na kuhudumu katika ibada hiyo.


 Kwaya ya watoto ya AICT Chang'ombe

 Kwaya ya wenyeji AICT Chang'ombe Choir



 Rose Jefa mwimbaji toka Kenya

 Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama

 Kwaya ya AIC Shinyanga 

 Wana LULU toka Mtoni

 MC Tito ndiye aliyeongoza jahazi 

 Keki ya miaka 25


 Hawa ni vijana wa kanisani hapo wenye umri wa miaka 25 waliobahatika kula keki hiyo.

 Mwenyekiti wa AICT Chang'ombe Choir akikata keki

 Walezi wa kwaya tangu kuanzishwa kwake

 Baadhi ya watunzi wa nyimbo zilizobeba albamu tangu kuanzishwa kwa kwaya hiyo.

 Askofu Salala akizindua jina jipya la AICT Chang'ombe Choir

Kikundi cha wagaratia wakipozi katika picha na watumishi wa Mungu

Thursday, December 5, 2013

KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA KUFANYA SHEREHE ZA JUBILEE YA MIAKA 25


Jumapili hii ni hekaheka, Katika viwanja vya K.K.K.T Kijitonyama, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama watakuwa na sherehe za kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake. Kwaya hii iliyoanzishwa miaka 25 iliyopita imejulikana sana kwa nyimbo zake zikiwemo Hakuna Mungu Kama Wewe, Simba wa Yuda, Hakuna Mwanaume Kama Wewe, Ndani ya Safina, Tone la Damu na Album yao mpya iliyoko sokoni inayofahamika kwa jina la Namtangaza Kristo. Sherehe hizo zitafanyika katika ibada ya tatu inayoanza saa nne asubuhi kanisani hapo na kisha kufuatiwa na tamasha kubwa litakaloanza saa saba mchana litakaloshirikisha kwaya kongwe toka Arusha maarufu kwa Jina la Tumaini Shangilieni toka kanisa la St. James Anglican lililoko Arusha na pia kwaya zote za kanisa la K.K.K.T Kijitonyama.

 Na kama haitoshi Kwaya ya Uinjilisti wataimba wimbo mmoja wa kwaya ya Tumaini Shangilieni na vivyo hivyo kwaya ya Tumaini Shangilieni kuimba wimbo mmoja wa Kwaya ya Kijito. Nyimbo hizi ni zile zenye majina ya Hakuna Mungu Kama Wewe.
Katika kuadhimisha tukio hilo kwaya ya Uinjilisti Kijito wataimba nyimbo zao za zamani (Enzi za Mwalimu) zilizotungwa tangu kwaya inaanzishwa, Pia wataimba na waimbaji wote wa zamani waliowahi kuimbia kwaya hiyo. Akiwemo Eliwinjuka, Albert Mafwenga, Joyce Kitale, Lilian Joshua Mlelwa na wengine wengi.
 Pia siku hiyo wanakwaya watagawiwa vyeti na kutunukiwa nishani za utumishi mwema tangu wale wa zamani na walio wapya walioimbia kwaya hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa kwaya ya Uinjilisti Kijito alisisitiza watu wafike wajionee wenyewe wasisubiri kusimuliwa. Na kwamba watu waje wajionee matendo makubwa ya Mungu aliyowafanyia katika kipindi cha miaka 25. Mwenyekiti alidokeza kuwa Kwaya zote siku hizo zitaimba LIVE CD zitasikilizwa nyumbani.