MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, October 29, 2012

CVC CHANG'OMBE WAZINDUA ALBUM YAO YA NNE

 Jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam maelfu ya watu walikusanyika katika viwanja hivyo kujionea uzinduzi wa album ya nne ya Chang'ombe Vijana Choir iliyopewa jina la USIKU WA MANANE. Mgeni rasmi akiwa ni mbunge wa Sengerema Mh. William Mganga Ngeleja. Uzinduzi huo ulioambatana na harambee ya uchangishaji wa Milioni za kitanzania 200, Rasmi na wageni wote waliofika walichangisha zaidi ya milioni 40, zikiwa ni fedha kwaajili ya kianzio cha ujenzi wa jengo la kitega uchumi cha kwaya hiyo kitakachojengwa maeneo ya Kijichi jiji Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo ambao umehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo askofu wa kanisa hilo la AICT dayosisi ya Shinyanga,na wachungaji,  pamoja na kwaya mbalimbali zikiwemo AIC Dar es salaam Choir kutoka Magomeni, Ukombozi Choir kutoka K.K.K.T Msasani, Majestic Singers kutoka E.A.G.T City centre, Neema Gospel Choir kutoka AIC Chang'ombe pamoja na Matendo Choir ya AIC Chang'ombe.

 Matukio Katika Picha

Kama linavyoonekana hapo juu, Ni jengo la kitega uchumi la kwaya ya CVC litakapokuwa limekamilika

 Matendo Kwaya ya A.I.C.T Changombe

 Mafundi mitambo wakiwa busy kuhakiki muziki unawafikia vilivyo wasikilizaji

 Mpiga picha za video wa CVC akiwa kazini

 Majestic Singers wakiwa wameketi kwa utulivu wakisikiliza yanayojri

 Neema Gospel Choir ya A.I.C.T Changombe wakilikamata jukwaa

 Huyu bwana mdogo wa kwaya ya  Neema Gospel Choir ya A.I.C.T Changombe alikonga nyoyo za watu kwa ustadi aliokuwa akiutumia kucheza

 Dar es Salaam Kwaya ya A.I.C.T Magomeni wakiwa busy jukwaani


 Majestic Singers toka E.A.G.T City Centre a.k.a Wazee wa kuotesha nyama kwenye mifupa
wakimtukuza Mungu jukwaani

 Nyomi lililofika kuona nini kinaendelea

 Kamati ya maandalizi wakiweka mambo sawa kabila ya uzinduzi

 Meza kuu walipokaa wangeni rasmi, Tokea kushoto ni askofu wa A.I.C.T Dayosisi ya Shinyanga akifatiwa na Mh. William Ngeleja (MB) na mgeni aliyemsindikiza

 CVC Haoo wakiingia jukwaani kwa style ya pekee wanakimbia kwa shangwe na vigelegele kuelekea jukwaani tayari kuizindua Album yao

 CVC Wakionesha namna jengo lao litakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika

 Wana CVC tayari tayari kwa kuimba

 wakisikiliza risala inayosomwa na mwenyekiti wa kwaya yao

 Mwenyekiti akisoma risala kwa mgeni rasmi

 Picha ya jengo hii hapa

 Mheshimiwa Ngeleja akijibu risala ya wana CVC

 Kwaya mbalimbali wakiwa wameketi wakisikiliza yanayojiri

 Askofu wa A.I.C.T Dayosisi ya Shinyanga akitoa maneno ya hekima

 Mheshimiwa William Ngeleja akizindua rasmi DVD ya USIKU WA MANANE kwa kukata utepe

 Jopo la wageni wazito wazito walioambatana na mgeni rasmi wakiwa tayari kusema yaliyoko mioyoni mwao katika kuchangia uzinduzi huo

 MC Machachari Bw. Tito akiweka DVDs tayari kwa mnada

 Mheshimiwa Ngeleja akiwakaribisha wageni alioambatana nao kuanza kutamka pledges zao

 Mch. Charles Mzinga toka K.K.K.T Azania Front  ni mmoja wa wachungaji waliokaribishwa katika uzinduzi huo
 Askofu toka Dayosisi ya Shinyanga ya kanisa hilo akisikiliza kwa makini

 Wageni toka nchi jirani ya Kenya nao wakimtolea Mungu

Wageni rasmi wakizawadiwa DVD za USIKU WA MANANE

Wednesday, October 24, 2012

KIJITO YETU WIKI ILOPITA

Mfululizo wa matukio yanayojiri katika Ibada K.K.K.T Kijito unaendelea, Wiki ilopita Ibada ya Kijito iliongozwa na Mch. Ernest Kadiva na Aliyesimama kwa ajili ya mkate wa kiroho alikuwa msaidizi wa Askofu, Mchungaji George Fupe ambaye alisisitiza watu kumtolea Mungu kwa moyo tunapoelekea katika kipindi cha mavuno tarehe 4 Novemba 2012. Katika ibada hiyo pia iliyopambwa na Praise Team walioongoza kipindi cha sifa na kuabudu.
Praise Team wakiongozwa na Allen Mwaipaja wakati wa kipindi cha PnW

Wapedwa wako busy katika kuabudu

Msaidizi wa Askofu, Mch Geoge Fupe akihubiri

Wadau wakapata nafasi ya kuombewa kabla hawajaanza maisha mapya ya ndoa, Tokea kushoto ni Bi Orpah Kiondo na mtarajiwa wake Elisha Mushaija na kulia ni Cuthbert Kagirwa na mke wake mtarajiwa

Wakapewa wazazi wa kiroho wa kuwa-guide katika maisha mapya

Kwaya ya vijana toka Azania Front wakiimba wakati wa ibada

Friday, October 19, 2012

VURUGU ZATANDA JIJINI DAR ES SALAAM

Baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick kuzuia maandamano yaliokuwa yamepangwa kufanywa  leo hii na waumini wa dini ya kiislam baada ya swala ya ijumaa, Nia yao ikiwa ni kuishinikiza serikali kumwachia sheikh Ponda na malalamiko mengine kama walivyoyaorodhesha.


Lakini baadae hali ya hewa ikaja kubadilika kwa waliokuwa wakaidi amri hiyo na kujikuta matatani, Pale jeshi la polisi lilipoamua kuingilia kati kuzuia vurugu hizo.
Kama inavyoonekana kwenye picha
 Mmojawapo wa waliokamatwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi

Wazee wa kazi wakilinda maeneo ya jiji
Ni ulinzi kila kona ya jiji

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa katika Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake kuimarisha ulinzi.

Mitaa ya Msimbazi Kariakoo
Maktaba House





Monday, October 15, 2012

Waislamu Washambulia Makanisa Dar, Wachoma na Kuharibu Magari

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema mtoto mmoja (mkristu jina tunalo) akiwa katika michezo na mwenzake wa Kiislamu walianza kubishana, kuwa endapo ukikojolea kitabu cha dini ya Kiislamu (msaafu) lazima ugeuke kuwa kichaa, hivyo Josephat alibisha na kumwambia mwenzake anaweza kufanya hivyo na kutodhurika.

Baada ya mabishano hayo Josephat aliamua kukikojolea kile kitabu ili aone kama angelidhurika kama alivyoelezwa na mwenzake, lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo baadaye yule wa kiislamu alitoa taarifa kwa wazazi wake ndipo yalianza mazungumzo kati ya wazazi kwa wazazi.

Kova alisema mvutano huo ulifika katika kituo kidogo cha polisi na ndipo baadhi ya Waislamu walianza kujitokeza na kutaka wapewe maelezo na kadri ya walivyoongezeka eneo la kituo hali ilianza kuwa mbaya kwani baadhi yao walionekana kutaka kufanya fujo na kuomba wapewe yule mtoto ili wamuadhibu.
Baada ya hali kuwa tete Jeshi la Polisi lilileta askari wa kutuliza ghasia FFU kuwataka waliokuwa kituoni kuondoka kwa amani lakini baadhi yao walipinga hivyo kuanza kutumia nguvu kuwatawanya. “Baada ya wananchi hao kutawanyishwa baadhi walijikusanya na kuzunguka huku wakifanya fujo kwa kushambulia Makanisa, Makanisa yalioshambuliwa ambayo yote ni ya maeneo ya Mbagala Kizuiani ni pamoja na Kanisa la Anglikana, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT-Mbagala) na Kanisa la Sabato ambayo yamevunjwa vioo pamoja na kuharibu mali kama magari yaliyokuwa yameegeshwa eneo la kanisa na mengine waliokutana nao waandamanaji hao.na mali za watu,” alisema Kova akizungumza na chombo kimoja cha habari.
K.K.K.T Mbagala ambalo ndilo lilioharibiwa

Mlango wa kanisa ukiwa umevunjwa vioo

Akina mama wenye mzigo wa maombi, wakiomba Mungu awarehemu waliofanya uharibifu huo

Vyombo mbalimbali vya kanisa hilo vilivyochomwa moto

Watu mbalimbali waliofika kanisani hapo kujionea uharibifu uliotokea

Gari la Mchungaji wa usharika hou wa Mbagala likiwa limeharibiwa vibaya

Jionee uharibifu uliofanywa


Kushoto unaonekana msikiti walipotokea waumini wa dini ya kiislamu kwenda kufanya uharibifu huo.

Dean Geoge Fupe msaidizi wa Askofu mkuu wa kanisa la K.K.K.T Alipofika kanisani hapo kuona kulichojiri

Viti vikiwa vimerushwa huku na kule

Mimbari ya kuhubiria inavyoonekana baada ya kuchomwa moto

Mlango wa kanisa hilo na vitu mbalimbali vikiwa katika hali ya kusikitisha

Ofisi ya Mchungaji ilionekana hivi baada ya kutiwa moto

Inasikitisha sana

Mchungaji George Fupe akizungumza na mchungaji wa Mbagala juu ya yaliyojiri