MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, March 24, 2014

JUMUIYA YA EBENEZER YAWAJALI WAJANE

Katika ibada iliyofanyika jana katika Kanisa la K.K.K.T Kijitonyama. Ikiongozwa na Mchungaji Msaidizi wa usharika wa Kijitonyama Mch. Prosper Kinyaha akisaidiana na Bw. Onai Seng'enge aliyekua kiongozi wa ibada hiyo na Petro Zakayo ambaye ndiye alikuwa mhubiri.
Jumuiya Maalum (Ebenezer) al maarufu kama Jumuiya Mchanganyiko kwa umoja wao wakiwa wameshikilia jahazi la ibada hiyo jana waligusa nyoyo za wajane kwa kutoa sadaka ya Vyerehani vinne pamoja na vifaa vyote vya ushonaji kwa kundi la akina mama wajane wa usharikani hapo. Akisoma risala Bw. Daudi Goodluck Daudi Alisema wameguswa kufanyanya hivyo ili kuinua kipato cha akina mama hao. Aidha alisema takribani milioni moja na nusu zilitumika katika upatikanaji wa vifaa.

Matukio katika picha:

 Bwana Onai Seng'enge akiwa madhabahuni akiongoza Ibada.

 Mchungaji Prosper Kinyaha Mchungaji Msaidizi wa Usharika wa Kijitonyama

 Mchungaji Prosper Kinyama akiwaombea watu walikuja kumshukuru Mungu kwa shukrani za Pekee
Aliyewekewa mikono  mkono wa kulia ni kijana Francis Malya (Macha)

 Kwaya ya Jumuiya Maalum wakimtukuza Mungu wakati wa ibada

 Bi Everlight akiongoza jahazi la kwaya ya Jumuiya Maalum.

 Kijana wa Jumuiya Maalum akisoma neno la Waraka

 Kijana wa Jumuiya Maalum akisoma neno la Mahubiri

 Mwanadada huyu wa Jumuiya Maalum akisoma matangazo ya Usharika

 Petro Zakayo akihubiri

 Mchungaji Ernest Kadiva, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama akitoa salamu.

 Bwana Daudi Goodluck Daudi Mwenyekiti wa Jumuiya Maalum akisoma Risala ya Jumuiya yao  Mbele ya washarika.

 Sehemu ya wana Jumuiya Maalum wakisikila kwa Makini wakati wa ibada.

 Maelfu ya watu waliofika kuabudu K.K.K.T Kijitonyama jana.

 Sehemu ya sadaka kwa wajane iliyotolewa na Jumuiya Maalum

 Tokea kulia mtu wa pili na wa tatu wakiwa wamejitokeza kuchangia sadaka kwa wajane

 Bi. Margaret Kamugisha akitoa tangazo juu ya Uchangiaji wa Huduma ya kupeleka Injili kusikofikika utakaofanyika katika Hotel ya Land Mark Ubungo tarehe 30/03/2014 Kuanzia saa nane Mchana.
Usikose mtu wa Mungu.

 Mwenyekiti wa Jumuiya Maalum Bw. Daudi Goodluck Daudi Akikabidhi kwa Mch. Ernest Kadiva, Sehemu ya vyerehani vinne pamoja na vifaa vya ushonaji vilivyotolewa zawadi kwa wajane wa Usharika wa Kijitonyama.

 Waonaonekana na nyuso za furana ni akina mama wajane wa Usharika wa Kijitonyama wakifurahia zawadi toka kwa Jumuiya Maalum baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo na Mch. Ernest Kadiva.

 Hivi ndivyo ibada ilivyoisha kwa maombi ya pamoja.