MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, May 9, 2011

Uinjilisti Kijito Wafanya Ziara ya Injili Makorora - Tanga

Kwa mara nyingine tena, Kwaya ya uinjilisti Kijitonyama ilipata kusafiri kuelekea Tanga kwa huduma ya injili katika usharika wa Makorora. 
Safari yao ilidumu kwa muda wa  siku 2 kwani waliondoka Dar es Salaam siku  ya jumamosi na kufanya huduma ya kuhamasisha harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la kanisa la Makorora siku ya jumapili. 
Katika safari yao waliambatana na mkuu wa kanisa la KKKT Askofu Alex Malasusa
Ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uhamasishaji katika harambee hiyo ambayo ilifana.

Hili ndilo basi walisosafiria hapa wakiwa wamefika njia panda ya Segera kupata japo soda
 
 Kama wanavyoonekana na uchovu kidogo wakisubiri soda ziletwe
 Likiwa katika mtazamo mwingine ni gari walilosafiria

Hapa wakipata soda


 Tayari wamechangamka tayari kuendelea na safari

 Kanisa ambalo walipokelewa kwanza kabla ya kufika Makorora

 Hili ndilo jengo la kanisa ambalo lilifanyiwa harambee ili ujenzi wake umalizike

 Kabla ya ibada hapa ilikuwa asubuhi kwaya wakikagua vyombo vyao kama viko salamabaada ya mvua kunyesha

 Juhudi binafsi ilibidi zitumike ili kukausha maji kwa kila njia

 Hatimaye mambo yakawa vema wakaanza injili kwa njia ya uimbaji

 Wakiimba kwa sauti ambazo zilisababisha kuhamasisha watu kumtolea Mungu


 Hivi ndivyo walivyojipanga stejini

 Mpiga kinanda akiwa katika utumishi

 Huyu nae akilipiga gitaa la solo kwa ustadi

 Mwimbaji akiimba wimbo maarufu wa ndani ya safina (anayepiga gitaa)

 Huyu ni kijana machachari katika kuzipiga drums

 Tumba zilikuwepo pia kwa rahaaaa akionesha ustad wake kijana huyu
 
 Baadhi ya wakristo walikuwepo katika ibada hiyo

 Kwaya ya Tumaini Makorora wakimtukuza Mungu

 Askofu Alex Malasusa akijadili na mkewe mama Erica Malasusa

 Askofu akiwasikiliza wa waumini waliokuwepo ibadani siku hiyo

 Tayari kabisa kupokea zawadi

 Hapa akipewa zawadi ya msalaba anaye mvalisha ni dada wa kimasai

 Askofu  akivalishwa nguo za kimasai

 Mama askofu naye akivalishwa nguo na urembo wa kimasai

Askofu akiifurahia zawadi

Tuesday, May 3, 2011

Naburudika

Toyelelo