MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, August 29, 2013

ASKOFU MOSES KULOLA HATUNAYE TENA


Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa watu wa ndani mwa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr. Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.

TAHARUKI YA BOMU K.K.K.T KIJITONYAMA MAJUZI

JUZI (Jumapili) Tarehe 25 Septemba 2013, hali ya taharuki ilizuka kwa waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam baada ya kuonekana kifaa cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kilichosadikiwa kuwa bomu.
Kifaa hicho ambacho kilifungwa katika boksi kilikutwa juu ya transfoma iliyoko nyima ya jengo la kitega uchumi cha kanisa hilo umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana, Mtabiri Mwandamizi wa TMA, Agustine Kanemba alisema kifaa hicho huwa kinarushwa kila siku kwenda angani kwa urefu wa kilometa 55,000 kikiwa kimeambatana na puto.
Alisema kikifika huko puto hupasuka na kusababisha kifaa hicho kudondoka chini jambo ambalo linasababisha wao kupata taarifa za hali ya hewa ya anga baada ya hatua hiyo. Lakini mara nyingi kifaa hicho hudondokea baharini.

 Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kijitonyama

 Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Hilo ambalo nyuma yake ndipo ilipo transformer kilipokuwa kifaa hicho kilichodhaniwa kuwa ni bomu.

 Hiki ndicho kifaa cha Mamlaka ya hali ya hewa TMA Kilichodhaniwa kuwa ni Bomu

 Mtaalamu akiangalia kifaa hicho

 Wataalamu hawa wakiondoa kamba iliyokuwa imefungwa kwenye kifaa hicho.

 Wataalam wakifanya bidii za kukitoa kifaa hicho kwenye transformer

 Tokea kushoto ni Michael Mwalwisi na Lukio Mjema wakikiangalia kifaa hicho kwa umakini

 Ni kama anasema....Jamani hili sio bomu ni kifaa cha kupimia hali ya hewa.

 Waumini na wananchi wakikiangalia kifaa hicho kwa karibu

 Waumini wakipata maelezo toka kwa mtaalamu kuhusiana na kifaa hicho.

 Watu wakifurahi baada ya kuhakikishiwa usalama wao

Watu wa Emergency wa kampuni ya umeme TANESCO walifika pia kuhakiki usalama.
 
Wakiondoka baada ya hali ya taharuki kutoweka

Wednesday, August 28, 2013

NEEMA GASPAL KUIBUKA NA ALBAMU YA SHUJAA

Neema Gaspal


Neema Gaspel Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Anategemea kuwa na Tamasha la Uzinduzi wa Album yake ya kwanza, Tamasha ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza siku ya Tarehe 1 Septemba 2013.

Album hiyo inayojulikana kwa jina la SHUJAA iliyobeba nyimbo nane ambazo ni:
1.Shujaa
2.Mweleze Yesu
3.Machozi Yako
4.Nimekukimbilia Bwana
5.Ee Mungu
6.Kristo
7.Faida
8.Kwa Neema

Neema Gaspel Akizungumza na Christian Bloggers (Hawapo kwenye Picha)
 Lengo kuu la uzinduzi huo likiwa ni kusaidia watoto yatima na wajane kwa asilimia Fulani ya kiasi kitakachopatikana siku hiyo, Huku akisindikizwa na waimbaji Rose Mhando, Bahati Bukuku, Madam Ruth, Martha Mwaipaja, Everine Msoma, Ambwene Mwasongwe, Mwanamapinduzi Maximilian Machumu, Edson Mwasabwite, Enock Jonan a Wengine wengi.
Mgeni rasmi Atakuwa Mh. Samuel Sitta Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Atakayeongoza jopo la wageni mbalimbali kuzindua na kumuunga mkono Neema.
Viingilio siku hiyo vitakuwa kama ifuatavyo.
Viti Maalum 10,000/=
Kawaida
Wakubwa 5,000/=
Watoto 2,000/=
Tiketi zinapatikana Praise Power Radio, Wapo Radio pia zitapatikana siku hiyo mlangoni siku ya tamasha. Watu 50 wa kwanza watapata zawadi kama Lotion kutoka kwa wadhamini wa tamasha hilo Grace Products. Pia Kutakuwa na Fashion Show pamoja na mashindano ya ngumi na kudance. Usipange kukosa.

JOSEPHINE MINZA NKILA KUTOKA NA VIDEO YA MAISHA YA IBADA


Josephine Minza Nkila
Mwanadada Josephine Minza Nkila ambaye mara nyingi uhudumu na Mwalimu Mgisa Mtebe wa huduma ya Robbon Ministries. Anategemea kuachilia Video yake mpya itakayokuja kwa jina la MAISHA YA IBADA (LIFE OF WORSHIP) tarehe 22 September 2013. Video hiyo ambayo imechukuliwa live katika Ukumbi wa Upanga City Christian Centre, mahali ambapo Video hiyo itazinduliwa hapo hapo pia. 

Akizungumza na waandishi wa habari Minza alisema video yake imesheheni jumla ya nyimbo 10 zenye maadhi ya slow (Worship Music), Kwaito na kadhalika.
Pia siku hiyo anategemea kupiga nyimbo zake katika mfumo wa LIVE Music.


Samuel Yona
 Akishirikiana na wanamuziki wafuatao:
Abednego Hango, Ipyana Kibona, Prisca Kangi, David Yona, Jenifer Mushi na Samuel Yona ambaye ndiye producer aliyeisuka album hiyo.

 Kama inavyoonekana katika picha hapo juu ni wakati video hiyo ikirekodiwa, Usikose siku hiyo.

 

Wednesday, August 7, 2013