MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, November 23, 2015

K.K.K.T KIJITONYAMA WASHEREHEKEA SIKU YA MAVUNO

Jana tarehe 22-11-2015 Ilikua siku ya pekee kwa Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kijitonyama wakisherehekea siku ya mavuno. Ambayo hufanyika kila mwaka. Wakifurahia siku hiyo walikuja katika nyumba ya ibada wakiwa wamebeba vinono vya shamba vikiwemo Ndizi, Vitunguu, Bilinganya, Nyanya, Ufuta, Maziwa na aina nyingine nyingi za Mavuno. Ibada hiyo iliyoongozwa na Mch. Anta Muro ambaye pia ni mkuu wa jimbo akishirikiana na Mch. Lameck toka Zanzibar. Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu wengi wakiwemo wenyeji na wageni. 

Fuatana nami ujionee matukio katika picha.


 Sehemu ya waimbaji wa Praise Team ya Usharika wakiimba wakati wa ibada.


 Tokea kushoto mwenye kitenge cha njano, ni Dr. Victoria Kisyombe, Nancy Buchcuski, Lilian Kinyaha na Mtui.


 Waumini waliohudhuria ibaya hiyo wakisikiliza kwa makini


 Wachungaji wakifanya maombezi wakati wa ibada.


 Mavuno kama yanavyoonekana kwenye picha


 Sadaka ya mavuno kama inavyoonekana vikiwemo vitunguu na ndizi.


 Ndizi zilizonona zilizoletwa kama sadaka ya mavuno.


 Vijana hawa Anderson akiwa na mwenzie wakiwa wameinyanyua juu ndizi ili ionekane kwa watu wote wakati wa kuibadilisha sadaka hiyo kuwa katika mtindo wa fedha.


 Mzee Nikubuka Shimwela akifanyama mnada.


 Mzee Nikubuka Shimwela akifanya mnada wa kuku.


 Wazee wa Usharika wakijitokeza kununua bidhaa hizo ili ziwe katika mfumo wa fedha.


 Baadhi ya wazee wa baraza wakisema ni nini wanamtolea Mungu .


 Mzee wa busara Charles Mwalongo akiwa tayari kutoa risiti kwa bidhaa zinazonunuliwa.


Kitengo cha mahesabu wakifuatilia na kutunza kumbukumbu.
 Wachungaji waliohudumu katika ibada, kutokea kushoto ni Mch. Lameck akiwa na Mch. Anta Muro.