MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, January 27, 2013

RACHEL SCHARP AZINDUA ALBUM YAKE

Mwana mama Rachel Scharp mtanzania aishiye nchini Sweeden, Jana majira ya jioni aliweka wakfu na kuzindua album yake iliyo katika mfumo wa cd yenye nyimbo kumi na dvd yenye nyimbo nane.
akifunguka mbele ya waandishi wa habari za kikristo, Rachel alikuwa na haya ya kusema.


Mimi ninaitwa Rachel Scharp, ni Mwimbaji  wa nyimbo za  Injili, ninaishi Malmo, Sweden. Lakini kwa sasa nipo nyumbani kwa ajili ya utambulisho wa Albamu yangu ya Muziki wa injili.
Uimbaji kwangu ni maisha kwa kuwa nilianza kuupenda muziki na kuimba  kuimba nikiwa mdogo sana, nilikuwa nikitunga nyimbo na kuwafundisha wadogo zangu. Tuliimba nyimbo hizo jioni, haswa kipindi kile cha ugawaji  ikiwa zamu ya Kaya yetu,  ile foleni ya kununua mchele  ilivyokuwa ndefu chakula kilikuwa kinachelewa, ili wadogo zangu wasilale bila kula na furaha ya kusubiria ubwabwa na maharage basi tunaimba kusubiria msosi, Wakati huo hakukiuwa na Tv. kama ilivyo sasa.

Niliimba Kwaya ya shule pale “Jangwani Secondary” pia niliongoza sifa na kuabudu Kwenye fellowship  katika kanisa la Msewe Lutheran . Nilikuwa nikiandika nyimbo nyingi nikitegemea kupata fursa ya kurekodi au kuimba na Kwaya nyimbo zangu, lakini sikupata fursa hiyo.

Kwa sasa ninaimba Kwaya kanisa la  Elim Pentecostal huko Malmo kusini mwa Sweden,  ninaongoza sifa na kuabudu. Ninaimba pia kwenye kundi linaloitwa Shalom International ambalo ni muunganiko wa waimbaji kutoka makanisa mbalimbali ya kiroho yaliyopo mjini Malmo. Nilipata fursa ya kurekodi album yangu ya kwanza mwaka 2008 ikazinduliwa huko Sweden,  Mai mwaka, 2009 nikisindikizwa na dada Upendo Kilahiro. Album hiyo niliita 'Naringa na Yesu' yenye nyimbo  9, iko Kwenye mfumo wa sauti tu.

Leo ninatambulisha album yangu ya pili yenye jina la 'Ni Mungu wa ajabu'. Album hii Ina nyimbo kumi zilizo Kwenye mfumo wa sauti (audio), na 8 Kwenye mfumo wa  picha na sauti (DVD).
Nimerekodi album hii Oktoba  mwaka 2011 nchini Sweden,  kwa upande wa mpangilio wa vyombo na muziki nikisaidiwa na Paalab Nyarko, kutoka Ghana na producer Zolile Matikinga(Zorro) - kutoka South Afrika.

Mwanzoni mwa mwaka 2012 niliongeza baadhi ya vionjo vya muziki kwenye studio za New Life band Arusha, vionjo nilivyoingiza ni  gitaa la solo lililopigwa na Godlucky Matingisa wa New life band Arusha, Base Gitaa limepigwa na Wilsson Godfrey Mtangoo.  Ngoma zilipigwa na Fujo Makaranga . Na sauti pia niliingiza hapo Arusha nikisaidiwa na Jackson Benty, chini usimamizi na uangalizi wa producer  Wilsson Mtangoo. Mwalimu wa sauti mchungaji David Nkone.

Video imerekodiwa na UMU production Arusha chini ya uongozi wa Jojo Jose Mwakajila. Video hii imerekodiwa Sweden (Malmo), Ujerumani (Berlin), Tanzania (Dar es Salaam, Bagamoyo, Arusha ,Moshi, Serengeti).

Midundo ya  nyimbo hizi ni ya  kiasili (kitamaduni), Napenda nyimbo zenye vionjo vya Kiafrika na kitanzania zaidi. Nimeimba kwa kiswahili na kiingereza pia. Na nyimbo nyingi ni za kiswahili, hii haimaanishi kwamba  soko liko nchi wanazoongea kiswahili tu. cha kushangaza ni kwamba pia nch za Scandinavia wanapenda sana kiswahili na kukithamini, na nafikiri kuliko hata sisi wenye lugha.
Wanasema kwamba ni lugha yenye sauti tamu nami sina budi kujivunia na kuiendeleza na huku nikimsifu Mungu na kupeleka ujumbe kwa Watu wake.

Nyimbo hizi zimebeba jumbe mbalimbali, kuna za kumsifu Mungu na matendo yake makuu, kuna za maonyo na kuna za kutia moyo kwa safari hii ngumu ya kwenda mbinguni.
Ningependa sana watu wapate ujumbe huu na wakutane na Mungu katika maeneo hayo tofauti kama nilivyoeleza mwanzoni  kuwa kuna kumsifu na  kumwabudu Mungu, kuonywa na kutiwa moyo pia. Inategemea mtu yuko kwenye hali gani na ana mahitaji gani.

WITO WANGU KWA JAMII

kwanza ni kupenda na kuthamini kile tulicho nacho Mungu alicho tupatia.
Kwanza kwa sisi wakristo tumepewa Neema hii ya wokovu tunatakiwa tuipende, tuithamini, tuitunze na tuiendeleze, tusiichezee na tuwafanye wengine pia waijue na waipate.
Kama tusipoipenda, tusipoithamini, kujivunia na kuilinda, wengine hawatajua thamani yake.

Nikaja kwenye jamii yetu kwa sasa tunapenda sana kuiga kutoka nje tunaacha ya kwetu, sikatai kuiga yale yaletayo maendeleo, na tunahitaji kujifunza kutoka kwa walioendelea, lakini si kwamba tuvipuuzie vya kwetu. Kuna vyetu vinavyohitaji mwendelezo.na tena vikawa vizuri  sana na wa nje wakaiga kutoka kwetu. Kwa Mfano;  muziki wetu , lugha yetu na vingine vingi.

Kwa upande wa muziki, watanzania siku hizi wanapenda sana muziki kutoka Afrika kusini, ni mzuri sana hata mimi napendezwa nao. Naona sasa waimbaji wengi wanapenda kupiga mtindo huo. Ule ni muziki wa asili wa ngoma zao za kienyeji ukawekwa/ukaongozewa vionjo vya kisasa.

Sasa na sisi tutakapopiga muziki huo hautakuwa mzuri kama wanavyopiga Joyous Celebration kwa kuwa ndio asili yao. Swali ni kwamba, kwa nini na sisi watanzania tusitengeneze lizombe letu au Mdumange au Sindimba na hata Mdundiko tukaweka vionjo vya kisasa ukawa mzuri tu na wao waige kutoka kwetu?
Nilazima tujitahidi jamani tuwe na utambulisho wetu (identity). Kwamba ukisikika muziki uutambue mmmh Huu ni muziki wa Tanzania, tunahitaji ubunifu tu kuondoa uvivu wa kufikiri. Kama tukitulia na kubuni na kutumia vipawa tulivyopewa na Mungu tutafika mbali sana na sio kupita njia ya mkato ya kuiga tu.
Namalizia kwa kuwaambia watanzania, tusiende kwa mazoea eti watu wamezoea hivi. Huu ni wakati wa mabadiliko, tubadilike turudi kwetu.  Tutafika mbali. watanzania tunaweza, na kuleta mabadiliko ni mimi na wewe.

Asanteni sana kwa kuja  kushiriki pamoja nami tukio hili la Baraka. Mungu awabariki sana.



Rachel Scharp

Yafuatayo ni matukio katika Picha wakati wa hafla hiyo:

 Master Prophet C J Machibya akifungua hafla hiyo kwa sala

 Rita Chuwalo ndiye alikuwa MC katika uzinduzi huo

 Waandishi wa habari za kikristo wakijitambulisha tokea shoto ni Luphurise Lema, Nice na Furaha

 Kizazi kipya katika muziki wa injili hiki hapa. 
Huyu ni mtoto wa Upendo Kilahiro akijitambulisha

 Yale yale mtoto wa... ni ... Huyo ni mtoto wa Ritha Chuwalo akijitambulisha

 Chezea Sam Sasali itakucost mwenyewe. 
Hapa yuko busy hata aking'atwa na mbu hola!

 Kama kawaida ya mzee wa Standup comedy King Chavala, uwepo wake tu lazima ucheke

 Mwenyewe Rachel Scharp ndo huyu hapa yuko busy ana-ipad-iika

 Rachel akiweka mambo sawa wakati akifanya utambulisho wa familia yake

 Rachel akiwatambulisha baba Mlezi na mama yake mzazi

 Hapa akimtambulisha mdogo wake (mwenye shati jekundu)

 Master Prophet CJ Machibya akiibariki na kuizindua rasmi
 DVD na audio CD za mwana mama Rachel

 Rachel akienda sawa jukwaani na vijana wa kazi

 Hapa DVD na CD zikiombewa tayari kwa kazi ya kuwavuta watu kwa Yesu

 DVD na CD ndo hizi hapa

 Upendo Kilahiro akienda sawa on the stage

 Chavala kama kawaida yake akiwavunja watu mbavu

 Uncle Jimmy akiwa busy kuchukua matukio

 Rulea Sanga akiwa na kitendea kazi mkononi

 Waandishi wa habari toka WAPO Radio FM na Clouds TV 
wakifanya mahojiano na Upendo Kilahiro pamoja na Rachel Scharp

 Camera mans wakifanya kazi zao.