MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, June 13, 2012

VIVA SHUSHO VIVA TANZANIA CAMPAIGN YABAMBA


Mpigie kura Christina Shusho ashinde tuzo ya Africa Gospel Music Awards 2012 Inayotolewa na AGMA. BOFYA HAPA



Watanzania:  
Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende. Ezra 10:4


Siku 18 zimebakia kabla ya pazia la upigaji kura kufungwa kwa waimbaji wa gospel barani Afrika, ambao wanawania tuzo mbalimbali kupitia Africa gospel music awards ambazo zinatarajiwa kutolewa siku ya jumamosi ya tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza. Ambapo kama ilivyokuwa kwa mwaka jana mwimbaji wetu mmoja tu, ametutoa kimasomaso kwa kupendekezwa katika kuwania kupata tuzo hizo mwimbaji huyo si mwingine bali ni Christina Shusho, ambaye mwaka jana alitoka mikono mitupu lakini mwaka huu tukiungana kwa pamoja watanzania wote kwa kumpigia kura lazima atarudi na tuzo zote mbili alizopendekezwa kuwania.

Shusho yumo kwenye kuwania mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na mwimbaji bora wa mwaka Afrika ya mashariki, tuzo ambazo anawania na waimbaji wengine wanaofanya vyema kwenye gospel barani Afrika wakiwemo wakina Ntokozo Mbambo wa Afrika ya kusini na waimbaji wengine. Kikubwa ninachoweza kukwambia tukifanikiwa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kwa kumpigia kura atakuwa nanafasi kubwa ya kutwaa tuzo hizo, kwasababu waimbaji wengine wanaowania tuzo hizo wengi wao wanatoka nchi moja hali ambayo itafanya kura zao kugawana kitu ambacho kitatupa nguvu ya kumwezesha Shusho kurudi na tuzo kwani Tanzania nzima kura zetu tunaelekeza kwake.


Mikakati mbalimbali inafanywa ili kuhakikisha kila mtu anashiriki katika upigaji kura kwakuwa hauhitaji kulipa ili kupiga kura, kikubwa unatakiwa ujiandikishe kwenye tovuti ya shindano hilo ambayo maelekezo yake yapo chini ya habari hii, zaidi kama nilivyoandika mikakati inafanywa ili kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili katika siku 18 zilizobaki. Hapo jana bloggers walikutana na Christina Shusho katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ili kupanga mikakati zaidi ya kuweza kupata tuzo hizo ambazo faida yake ni kumwinua Yesu pamoja na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania duniani. Natumai umenielewa ili kupiga kura ingia kwenye link hii na kufuata maelekezo chini yake.


http://www.africagospelawards.com/nominate.html

VOTE NOW
AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the 'VOTE NOW' button.

2. Register your email address, confirm and submit.

3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.

4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.

5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category). 

6. You do not have to vote in every category.



  MATUKIO KATIKA PICHA BAADHI YA 
CHRISTINA BLOGGERS (CBs) NA CHRISTINA SHUSHO JANA 

Christina Shusho, akiwasikiliza CBs kwa makini
Papaa akitupia neno kati kwa Tina Shusho wakati akimwelezea nini CBs wanafanya katika kuhakikisha zoezi zima la kumpigia kura mzaliwa wa kwanza wa Tanzania katika AGMA
Shusho, Martin Malecela pamoja na Victor Mboya wakisikiliza kwa makini mpango mzima.
Rulea Sanga nae alikuwepo
Mbinu za uwezeshaji zikisikilizwa.
K-junior wa kwanza kuume hadi akitabasamu jinsi mbinu zinavyopangwa.
Hakika kikao kilinoga wajameni.
Unclejimmy yeye aah akaanza hapo hapo kuwatumia watu meseji ili wapige kura.