MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, March 29, 2011

keronyingi.blogspot.com: Ya Loliondo yatokea Tabora pia.

keronyingi.blogspot.com: Ya Loliondo yatokea Tabora pia.: "Umati wa watu wakiwa wamepanga foleni ili kupata kikombe cha dawa Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora mjini am..."

Thursday, March 10, 2011

SERIKALI YASITISHA TIBA YA MCH. MWASAPILE

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima kuzuia haraka matibabu ya magonjwa sugu yanayoendeshwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo.

Dk Mponda alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua matumizi ya Bajaji kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa. Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumzuia mchungaji huyo kuendelea na utoaji wa dawa mpaka serikali itakapojiridhisha na hali ya usalama pamoja na uwezo wa dawa hiyo.

“Kutokana na hali halisi ya usalama wa kiafya kwa sasa katika eneo hilo, kuna hatari ya kuwepo kwa milipuko ya magonjwa kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka,” alisema Dk Mponda.

kwa habari zaidi 
BOFYA HAPA


 Foleni kuelekea kwa Mchungaji Mwasapile

 Umati wa watu waliofika kijijini kwa Mch. Mwasapile wakisubiri kupata huduma

 Dawa ikichemshwa

Dawa iliyochemshwa tayari kwa kunywa

Mchungaji Mwasapile akitoa dose

Watu mbalimbali waliofika kijijini huko

Mapumziko baada ya kupata dawa