MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, October 29, 2012

CVC CHANG'OMBE WAZINDUA ALBUM YAO YA NNE

 Jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam maelfu ya watu walikusanyika katika viwanja hivyo kujionea uzinduzi wa album ya nne ya Chang'ombe Vijana Choir iliyopewa jina la USIKU WA MANANE. Mgeni rasmi akiwa ni mbunge wa Sengerema Mh. William Mganga Ngeleja. Uzinduzi huo ulioambatana na harambee ya uchangishaji wa Milioni za kitanzania 200, Rasmi na wageni wote waliofika walichangisha zaidi ya milioni 40, zikiwa ni fedha kwaajili ya kianzio cha ujenzi wa jengo la kitega uchumi cha kwaya hiyo kitakachojengwa maeneo ya Kijichi jiji Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo ambao umehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo askofu wa kanisa hilo la AICT dayosisi ya Shinyanga,na wachungaji,  pamoja na kwaya mbalimbali zikiwemo AIC Dar es salaam Choir kutoka Magomeni, Ukombozi Choir kutoka K.K.K.T Msasani, Majestic Singers kutoka E.A.G.T City centre, Neema Gospel Choir kutoka AIC Chang'ombe pamoja na Matendo Choir ya AIC Chang'ombe.

 Matukio Katika Picha

Kama linavyoonekana hapo juu, Ni jengo la kitega uchumi la kwaya ya CVC litakapokuwa limekamilika

 Matendo Kwaya ya A.I.C.T Changombe

 Mafundi mitambo wakiwa busy kuhakiki muziki unawafikia vilivyo wasikilizaji

 Mpiga picha za video wa CVC akiwa kazini

 Majestic Singers wakiwa wameketi kwa utulivu wakisikiliza yanayojri

 Neema Gospel Choir ya A.I.C.T Changombe wakilikamata jukwaa

 Huyu bwana mdogo wa kwaya ya  Neema Gospel Choir ya A.I.C.T Changombe alikonga nyoyo za watu kwa ustadi aliokuwa akiutumia kucheza

 Dar es Salaam Kwaya ya A.I.C.T Magomeni wakiwa busy jukwaani


 Majestic Singers toka E.A.G.T City Centre a.k.a Wazee wa kuotesha nyama kwenye mifupa
wakimtukuza Mungu jukwaani

 Nyomi lililofika kuona nini kinaendelea

 Kamati ya maandalizi wakiweka mambo sawa kabila ya uzinduzi

 Meza kuu walipokaa wangeni rasmi, Tokea kushoto ni askofu wa A.I.C.T Dayosisi ya Shinyanga akifatiwa na Mh. William Ngeleja (MB) na mgeni aliyemsindikiza

 CVC Haoo wakiingia jukwaani kwa style ya pekee wanakimbia kwa shangwe na vigelegele kuelekea jukwaani tayari kuizindua Album yao

 CVC Wakionesha namna jengo lao litakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika

 Wana CVC tayari tayari kwa kuimba

 wakisikiliza risala inayosomwa na mwenyekiti wa kwaya yao

 Mwenyekiti akisoma risala kwa mgeni rasmi

 Picha ya jengo hii hapa

 Mheshimiwa Ngeleja akijibu risala ya wana CVC

 Kwaya mbalimbali wakiwa wameketi wakisikiliza yanayojiri

 Askofu wa A.I.C.T Dayosisi ya Shinyanga akitoa maneno ya hekima

 Mheshimiwa William Ngeleja akizindua rasmi DVD ya USIKU WA MANANE kwa kukata utepe

 Jopo la wageni wazito wazito walioambatana na mgeni rasmi wakiwa tayari kusema yaliyoko mioyoni mwao katika kuchangia uzinduzi huo

 MC Machachari Bw. Tito akiweka DVDs tayari kwa mnada

 Mheshimiwa Ngeleja akiwakaribisha wageni alioambatana nao kuanza kutamka pledges zao

 Mch. Charles Mzinga toka K.K.K.T Azania Front  ni mmoja wa wachungaji waliokaribishwa katika uzinduzi huo
 Askofu toka Dayosisi ya Shinyanga ya kanisa hilo akisikiliza kwa makini

 Wageni toka nchi jirani ya Kenya nao wakimtolea Mungu

Wageni rasmi wakizawadiwa DVD za USIKU WA MANANE

No comments:

Post a Comment