MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, March 27, 2012

HARAMBEE YA UJENZI WA CHAPLE MZUMBE UNIVERSITY YAFANA

Ilikuwa juzi jumapili, Harambee kubwa ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya ibada ya umoja wa makanisa ya C.C.T katika chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro. Harambee hiyo ilifana sana ikiongozwa na mgeni rasmi Prof. Josephat Kuzilwa akishirikiana na msaidizi wake Prof. Kamuzola. Pia kupambwa na kwaya mbalimbali mbali zilizokuwepo siku hiyo ikiwa ni pamoja na wenyeji kwaya ya U.C.F, Kwaya toka Mazimbu na kwaya toka Dar-es- Salaam Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama. Bila kusahau mshereheshaji wa shughuli hiyo alikuwa ni MC Shibanda wa Mwashibanda wenyewe wanamwita mzee wa haki ya Mungu.


Mambo yalikuwa kama ifuatavyo:

 Hili ndilo jengo ilipofanyika ibada hiyo ikifuatiwa na harambee


 Kwaya ya wenyeji wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe inayojulikana kwa jina ya U.C.F


 Walipendeza sana huku wakiiteka mioyo ya wasikilizaji waliokuwepo katika ibada hiyo


 Ni wazuri kwa steps na kucheza kama wanavyoonekana kwenye picha hapo juu.


 Katika mtazamo mwingine wakiwa humbled


 Prof. Kuzilwa akiongozwa kwaya yake jukwaani, Huyu prof. Yuko talented you cant believe MC Shibanda anasemaga 'Haki ya Mungu'


 Katika mwonekano mwingine walitokelezea ki hivi


 Kwaya ya Uinjilisti wakiwa wameliteka jukwaa kwa nyimbo za mapambio


 Hapa wakicheza style yao ya kupiga gitaa wakiongozwa na mwana mama MJ


 Drummer Boy Moses a.k.a Zinganoo akiipiga drums kwa umahiri


 Kijana Michael hakusita kukipapasa kinanda kikatoa sauti za kuvuti


 Dr. Tuntufye Mwamugobole mzee wa magitaa yote, this tym akatoka na gitaa la rhythm 


 Micah Songo yeye alikamata gitaa la solo, Anapiga gitaa huyu mpaka mlio wa nyau anaweza kukupigia


 M.C Onai ye aliamua kutoka na tumba


 Hii ndivyo high table ilivyosheheni wahshimiwa, Wachungaji na mgeni rasmi wa harambee


 Mchungaji aliyehubiri akihamasisha watu kutolea Mungu kwa moyo katika ujenzi wa nyumba ya Mungu


 Mwenyewe M.C Shibanda aliyekataa kuongoza shughuli mpaka avae koti kwanza


 Hapa ni baada ya kulivaa koti na kuanza shughuli ya kusherehesha vema, ni kama anasema " Haki ya Mungu nimependeza"


 M.C Shibanda akimkabidhi mgeni rasmi shughuli ya harambee huku akisisitiza mimi ni nani hata nisimame na mtu mzito kama huyu?


 Prof. Kamuzola nae akajitokeza na kutamka dau lake katika kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mungu


 M.C Foma foma akaomba kupiga picha na Prof. Huku akisema chance kama hizi zinatokeaga kwa nadra hivyo ukiipata itumie vema


 Hawa ni kina dada wa kwaya ya uinjilisti wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhudumu


 Mdau Tina (aliyesuka rasta) nae akaomba kutokelezea na rafiki yake kwenye blog


 Hii ilikuwa ni ibada ya usiku wa jana yake jumamosi, wana U.C.F wakiwa jukwaani wakiimba nyimbo za Tenzi za Rohoni


 Sifa zikavuma zikiongozwa na na mwanasifa wao


 Upako uliposhuka watu wakajiachia mbele za Bwana


 Hivi ndivyo walivyoonekana watu wote waliokuwepo kwenye Hall wakiabudu


Dada huyu wa kwaya ya uinjilisti Kijito anayefahamika kwa jina Jane aliwafurahisha watu kwa umahiri wake wa kuzipiga tumba

1 comment:

  1. Nimewakumbuka sana wapendwa!!!!Mungu azidi kuwabariki.Kazi nzuri kaka yangu.

    ReplyDelete