Jumapili hii ilikuwa ya aina yake, Pale usharika wa kijito uliposherehekea siku ya matawi ya mitende, habari za matawi ya mitende utazipata katika kitabu cha Yohana 12 Lakini kwa ishara tu jisomee hapa Yohana 12:13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli! Kwa sifa na shangwe kubwa na mapambio washarika walimsifu Mungu na baadae kufuatiwa na ujumbe wa neno la Mungu uliotolewa na msaidizi wa Askofu Mch. George Fupe akisisitiza kuwa mtende ni alama ya uhai furaha na amani.
Jionee matukio katika picha kama yalivyochukuliwa na blogger wetu.
Praise Team ya Kijito on the stage kwa furaha na matawi ya mitende juu kabisa wakiongozwa na Allen Mwaipaja
Hawa ni baadhi ya wanakwaya wa kwaya ya Uinjilisti Kijito pamoja na wale wa kwaya ya Vijana Kijito wakisifu na kucheza wakati wa kipindi cha sifa
Sehemu ya washarika wakiwa katika hali ya kucheza na kusifu huku matawi ya mitende yakiinuliwa juu
Kwaya Kuu nao hawakubaki nyuma katika kumsifu Mungu
Kikundi cha matarumbeta (waliovaa pink) lakini pia Waziri Mkuu mstaafu wa pili kutoka kulia wakimsifu Mungu kwa pamoja
Katibu wa baraza la wazee wa usharika wa Kijitonyama mwenye suti nyeusi na scarf nyekundu akiwa na uso wa furaha wakati wa ibada ya kusifu
Msaidizi wa Askofu, Mch. George Fupe wakati akitoa neno huku akifundisha maana ya matawi ya mitende
Kwaya Kuuu ya Usharika wakimsifu Mungu wakiongozwa na Mwl. Joachim Kisasa
Michael Karata alitoa shukrani siku hiyo akimshukuru Mungu kwa mambo mengi ambayo Mungu amemtendea na katika kipindi kigumu alichopitia mke wake
Waziri mstaafu Fredrick Sumaye akiwashukuru washarika wa Kijitonyama kwa kujitokeza katika harambee ya ujenzi wa usharika wake wa Makuruge
Mama Selina Mkonyi akiwahamasiha washarika kujitokeza na kuchukua fomu za kuchangia harambee ya kumalizia ujenzi wa kitega uchumi
No comments:
Post a Comment