MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, December 5, 2013

KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA KUFANYA SHEREHE ZA JUBILEE YA MIAKA 25


Jumapili hii ni hekaheka, Katika viwanja vya K.K.K.T Kijitonyama, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama watakuwa na sherehe za kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake. Kwaya hii iliyoanzishwa miaka 25 iliyopita imejulikana sana kwa nyimbo zake zikiwemo Hakuna Mungu Kama Wewe, Simba wa Yuda, Hakuna Mwanaume Kama Wewe, Ndani ya Safina, Tone la Damu na Album yao mpya iliyoko sokoni inayofahamika kwa jina la Namtangaza Kristo. Sherehe hizo zitafanyika katika ibada ya tatu inayoanza saa nne asubuhi kanisani hapo na kisha kufuatiwa na tamasha kubwa litakaloanza saa saba mchana litakaloshirikisha kwaya kongwe toka Arusha maarufu kwa Jina la Tumaini Shangilieni toka kanisa la St. James Anglican lililoko Arusha na pia kwaya zote za kanisa la K.K.K.T Kijitonyama.

 Na kama haitoshi Kwaya ya Uinjilisti wataimba wimbo mmoja wa kwaya ya Tumaini Shangilieni na vivyo hivyo kwaya ya Tumaini Shangilieni kuimba wimbo mmoja wa Kwaya ya Kijito. Nyimbo hizi ni zile zenye majina ya Hakuna Mungu Kama Wewe.
Katika kuadhimisha tukio hilo kwaya ya Uinjilisti Kijito wataimba nyimbo zao za zamani (Enzi za Mwalimu) zilizotungwa tangu kwaya inaanzishwa, Pia wataimba na waimbaji wote wa zamani waliowahi kuimbia kwaya hiyo. Akiwemo Eliwinjuka, Albert Mafwenga, Joyce Kitale, Lilian Joshua Mlelwa na wengine wengi.
 Pia siku hiyo wanakwaya watagawiwa vyeti na kutunukiwa nishani za utumishi mwema tangu wale wa zamani na walio wapya walioimbia kwaya hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa kwaya ya Uinjilisti Kijito alisisitiza watu wafike wajionee wenyewe wasisubiri kusimuliwa. Na kwamba watu waje wajionee matendo makubwa ya Mungu aliyowafanyia katika kipindi cha miaka 25. Mwenyekiti alidokeza kuwa Kwaya zote siku hizo zitaimba LIVE CD zitasikilizwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment