MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, May 28, 2012

TAMASHA LA KUCHANGIA USIKIVU MZURI WA RADIO YA UPENDO LAFANA

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi mchango wa sh. mil. 10 kwa Mchungaji George Fute ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu Alex Malasusa wakati wa hafla ya kuhitimisha harambee ya kuboresha usikivu wa Redio ya Dini ya Upendo 107.7 FM yenye lengo la kuchangisha na kupata kiasi cha sh. Mil. 220 iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
 Mchungaji George Fute ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu Alex Malasusa akitoa shukrani kwa Mgeni wa Heshima katika hafla hiyo ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa mara baada ya kukabidhi mchango wake pamoja na marafiki zake wa sh. Mil. 10 kwa ajili ya kuboresha na kuongeza wigo mpana wa kusikika kwa Redio ya Upendo FM.

Mheshimiwa Edward Lowasa mgeni maalum akisalimiana na Askofu mstaafu Elinaza Sendoro wa K.K.K.T

 Mh. Lowassa akiongoza zoezi zima la uchangishaji wa fedha kwa watu mbali mbali waliofika ukumbini hapo kw ajili ya kuichangia Redio Upendo FM. 
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake fupi kabla ya kukabidhi mchango wake na kuongoza harambee hiyo iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpongeza Mwanamuziki wa Ijili kutoka nchini Kenya,Sarah K ambaye alishirikiana nae katika zoezi la kuchangisha fedha hizo.
 Mchungaji George Fupe ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu Alex Malasusa akizungumza machache kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Askofu Mkuu ambaye hakuweza kufika kwenye hafla hiyo.
 Meneja wa Redio Upendo FM,Agatha Lema akisoma hotuba katika hafla hiyo.
 Meneja wa Redio Upendo FM,Agatha Lema akiikabidhi hotuba hiyo kwa Mgeni Rasmi.

 Muimbaji wa Muziki wa Injili kutoka nchini Kenya,Sarah K akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
 Muimbaji wa Muziki wa Injili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo,Faraja Ntaboba akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
 Muimbaji wa Muziki wa Injili ,Jennifer Mgendi akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
Muimbaji wa Muziki wa Injili,Joshua Mlelwa akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia waumini waliofika ukumbini hapo.
Kwaya Kutoka K.K.KT Azania Front
Kwaya toka K.K.K.T Vetenary
 Vikundi vya Kwaya mbalimbali. 
Bwana Lenard Shayo akiwa na wageni toka USA Jimbo la Michigan Nancy Buchkuski, Joan Patacony wakiwa na mdau Julieth Mutabiilwa
Watu mbalimbali waliofika katika tamasha hilo

picha kwa hisani ya michuzi blog

1 comment: