MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, May 15, 2012

TAMASHA LA KWAYA ZA UINJILISTI NA UAMSHO DAR ES SALAAM LAAMSHA NYOYO ZA WATU

Hapo jana katika jimbo la Kaskazini(zamani Kinondoni) la kanisa la Kilutheri dayosisi ya mashariki na pwani kumefanyika matamasha mbalimbali yanayoshirkisha kwaya za Uinjilisti na Uamsho(UKUU),moja ya vituo ilikuwa usharika wa Manzese jijini Dar es salaam ambako kwaya za Uinjilisti Sayuni kinondoni,Kijitonyama,Kawe,Hannanasifu,Mwananyamala na Manzese,  ziliweza kumsifu Mungu kwa pamoja huku kwaya tatu ambazo nazo zilipangiwa katika kituo hicho hazikufika.

Tamasha hili lilifunguliwa rasmi kwa maombi yaliyoongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo la Manzese,kisha kufuatiwa na uimbaji uliofunguliwa na kwaya ya Uinjilisti Sayuni Kinondoni na kuhitimishwa na kwaya ya Uinjilisti Manzese, Kilichowavutia watu zaidi ni jinsi ambavyo kwaya ya Uinjilisti Kawe ambao kila kukicha wamekuwa wakiongeza kiwango cha uimbaji,zamani kwaya hii ilikuwa imepewa jina la utani kwa kuitwa wanajeshi kutokana na waimbaji wake wengi kuwa wanajeshi kutokana na eneo walipo.Kisha kwaya ya Uinjilisti Kijito ambao watu walipendezwa na namna ya mpangilio wao wa muziki ulivyokuwa mzuri lakini pia na uchezaji wao. Sayuni hawakuwa nyuma wakiongozwa na soloist wao Balisidya aliyekonga nyoyo za watu jinsi alivyokuwa akicheza na sauti. Umoja huo wa kwaya za Uinjilisti na Uamsho(UKUU)umekuwaa ukifanya matamasha mara mbili kwa mwaka,mwezi wa tano kwa kuzigawanya kwaya katika makundi na tamasha la mwezi wa nane kwaya zote zaidi ya 15 zinakutana pamoja kwa uimbaji na kubadilishana vipawa.


 BAADHI YA MATUKIO KATIKA PICHA


Picha ya Kanisa la Lutheran Manzese baada ya ibada ya iliyofanyika asubuhi
 
Kwaya mbalimbali na washarika wakiwa tayari kwa tamasha


Wenyeviti wa kwaya mbalimbali zilizokuwepo wakitambulishwa na kiongozi wa UKUU


Mchungaji wa usharika akiongea neno la ufunguzi wa tamasha hilo









Waite Sayuni wazee wa Kinondoni ndio waliofungua tamasha
Wazee wa nguo za asili ndo wenyewe

Wanamuziki wa Kwaya hiyo wakiwa wanavicheza vyombo vyao vya muziki

Kwaya ya Hananasifu wakiwa jukwaani ndani ya BnW (Black and White)
Hawa ni Teule Mwananyamala ndio jina lao wakijishughulisha jukwaani
Katika mtizamo mwingine walionekana hivi

Fundi Mitambo Lukio Mjema akiwa kwenye mixer akiweka mambo sawa
 
Modest Mogan akiongoza sifa wakati wa matoleo

Uinjilisti Kijito wakisebeneka kwenye jukwaa

Jopo la wanamuziki wa Kijito wakivipapasa vyombo vyao

Anaye lead wimbo ni Gerald John, mwite Big ndo nick name yake ama (the voice)

Allen Mwaipaja akilitumia gunzi vema

Mwana dada Violet Mshiu wa Revocatus
 (aliyenyoosha kidole juu) akiimba kwa hisia

Shoto ni Eugene Mwamwembe akiwa na Kutyferra wakivicheza vinanda




Uinjilisti Kawe on the stage

Mwalimu Elidadi akiwaweka sawa waimbe kwa ustadi kama walivyolitawala jukwaa

Kawe wakiwa smart stejini

Hatimaye Calvary Manzese wakafunga dimba, 
Wanamuziki wa Manzese wakianzisha wimbo

Calvary Manzese kwa ujumla wao wakiwa kwenye steji

Washika magunzi wa Manzese wakifanya makamuzi

2 comments:

  1. Nice event, God bless everyone who participated and those who posted these events. Amen

    Vale Kamugisha

    ReplyDelete
  2. Hongereni watumishi kwa kumuinua Kristo Yesu! Mungu awabariki sana na muendelee kumsifu Mungu wetu aliye hai!

    ReplyDelete