MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, June 9, 2011

Kijito wiki hii

Wapenzi wa Blog hii. Naomba radhi kwa kuwacheleweshea matukio ya wiki iliyopita. 
Ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Nimewaletea matukio kwa njia ya 
video na matukio kwa njia ya picha yakuwa hewani muda si mrefu.

Yafuatayo ni matukio kwa njia ya video Utaona watoto wa Kijitonyama Sunday School
walivyoonesha kwa washarika jinsi walivyokuwa wamejiandaa kwenda katika tamasha la watoto lililofanyika jumapili iliyopita tarehe 5 June katika usharika wa Magomeni Mviringo. Pia utaona moja ya kwaya iliyohudumu kwenye ibada ya siku hiyo. Nayo si nyingine ni kwaya ya Uinjilisti ya usharika huo. Wakiimba wimbo wa nakimbilia msalabani.

Hivi ndivyo linavyonekana K.K.K.T Kijito


 Hivi ndivyo watoto wa Sunday School ya Kijito walivyoonesha vipaji vyao

 Mchungaji Kadiva akisema neno baada ya watoto kuimba

 Hatimaye waliombewa baraka ili wakauwakilishe vyema usharika

 Mdau Phesto Mwakyusa toka Ughaibuni akikabidhi zawadi kwa usharika toka ufini.

 Bwana Lenard Shayo alikuwepo kuzipokea akisaidiana ma mchungaji wa usharika

 Kwaya kuu ya usharika nao walikuwepo ndani ya nyumba

 Kwaya ya Uinjilisti wakihudumu ibadani siku hiyo

 Kwaya ya Uinjilisti wakiwa katika mtizamo mwingine


Nakimbilia Msalabani

 Haya sasa Ule wakati wa PnW (Praise and Worship) Ukiwa umeshika hatamu





 Mchungaji akisema jambo fulani kuhusu wadau hao. kama picha inavyosema

 Ndo ibado inaishiaishia hivyo

 Shoto ni Mwalimu Kisasa mtaalam na mwongoza uimbaji wa nyimbo hapo usharikani
 Mambo hayakuwa haba siku hiyo kijana Aggrey alipoamua kufunga ndoa

 Tabasamu la ukweli linaonekana jamani
 Anatafakari tu raha aliyonayo moyoni hakuna ajuaye ila yeye tu!

Step by step akiuelekea mlango wa kanisa tayari kwa ibada ya kufunga ndoa

1 comment:

  1. Asante kaka kwakutukumbusha haya!! Mchungaji mama Mbowe yuko usharika gani sasa hivi na Mchungaji Hiza jee?. nimekumbuka nyumbani.

    ReplyDelete