MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, March 4, 2013

UPENDO NKONE ANG'ARA TAMASHA LA PASAKA



MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Upendo Nkone ni miongoni mwa wasanii wa ndani watakaopamba Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Upendo anakuwa msanii wa tatu wa ndani kutangazwa atashiriki katika tamasha hilo baada ya Rose Muhando na John Lissu ambao walitangazwa Ijumaa na Jumamosi.


Akizungumza Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema mwaka huu katika tamasha hilo wanawapa mashabiki kile wanachokitaka."Tunaendesha maoni kwa mashabiki wetu wapendekeze wasanii gani wawepo, hivyo hao watatu ndiyo mpaka sasa wameshika nafasi za juu kwa kupendekezwa sana na mashabiki.

Wengine tutawatangaza kadri mambo yatakavyokuwa mazuri na pia tukiwa tumezungumza nao juu ya ushiriki wao,"alisema Msama.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31, kisha siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, Aprili 3 itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri Dodoma na Aprili 7 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
 

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava,

Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

 Picha ya wasanii na choir zilizohudumu Tamasha la pasaka mwaka 2012

Habari kwa hisani ya blog ya michuzi, www.issamichuzi.blogspot.com

No comments:

Post a Comment