MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, April 14, 2011

Ibada ya Kwaresma Kijito

Ikiwa imebaki wiki moja kabla ya siku kuu ya pasaka. Kama ilivyo ada ya usharika wa Kijito kuwa na ibada siku za jumatano kipindi cha kwaresma. Jana ibada hiyo iliongozwa na kwaya ya Uinjilisti ikiwa ni moja ya ratiba ya vikundi vya kwaya kuratibu ibada hizo kwa zamu. Ibada iliongozwa Na Joyce Nicholaus kwa ushirikiano wa Allen Mwaipaja ambaye ndiye alikuwa mhubiri na wazee wa zamu Godwin Manyiga, Modesta Mirisho na Suzan Mahenya. Pamoja na kwaya ya uinjilisti kwa ujumla ambao ndio walihudumu kwa njia ya nyimbo.
Fuatana nami katika matukio haya.

 Allen Mwaipaja akihubiri

  Joyce Nicholas ambaye ndiye aliongoza Ibada
 
 Sehemu ya wanakwaya wa kwaya ya uinjilisti walikuwe ibadani

 Upande mwingine wa wanakwaya

 Tokea kushoto niGodwin Manyiga, Suzan Mahenya na Modesta Mirisho
hawa ndio walihudumu kwa upande wa wazee wa zamu

 Sehemu ya washarika waliohudhuria ibadani


  Hivi ndivyo walivyoonekana watumishi wakiwa madhabahuni

 Kwaya wakihudumu kwa uimbaji

 Kiongozi wa ibada akiwaongoza watu kuomba

 Watumishi wakiwa "wamesimama kwenye zamu zao"

 Mtumishi huyo ndani ya joho. Utamjua?

 Mmmmh! Umeuvaa uhusika utadhani una experience ya miaka mingi
Mungu akubariki kwa utumishi wako wa jana.

 Wakiwa nje tayari kwa kumaliza ibada

 Enendeni kwa amani ya Bwana

 Wazee wa zamu wakiagana na kupongezana kwa utumishi


 Hongereni jamani! Zamu tumeimaliza

Wazee wa zamu wakiwa na watumishi katika picha ya pamoja

1 comment:

  1. Mungu awabariki sana wana kijito kwa mambo mengi ya kiusharika mnayoyafanya ili kuuinua usharika wenu. Niwatie moyo kwa kusema maneno katika Biblia yasemayo ''Taabu yenu si bure'

    ReplyDelete