Mchungaji
wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jijini Dar es
Salaam Paul Safari (katikati) alisema kuwa mkesha kama huwa unafanyika
pia katika nchi nyingi za Afrika, kama vile Kenya, Rwanda. Kauli Mbiu ya
mwaka 2012 ni kutoka zaburi ya 68:1 'Lets God Arise'. Mkesha huu
unaundwa na waimbaji zaidi ya 50 kwa kutengeneza timu moja yaani "Praise
Team" na hakutakuwa na waimbaji binafsi.
Mchungaji
wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jiji Dar es Salaam Abel
Orgenes (katikati) akionyesha kauli mbiu ya mkesha huo ambao unasema, 'Lets
God Arise'. Pembeni yake anayeshuhudia ni mchungaji Paul Safari (kulia)
na Samuel Mwangati (kulia) ambaye ni Music Director wa Aflewo.
Kwa upande wake Samuel Mwangati ambaye ni Music Director wa Aflewo alisema kuwa madhumuni ya Mkesha huu ni kama ifuatavyo.
1. Kuwaungaisha Wakristo Kutoka madhehebu yote katika Kusifu na Kuabudu.
2. Kuwaleta Pamoja wakrtisto Kuomba kwa ajili ya Kuliombea Taifa la Tanzania na Bara la Africa kwa ujumla.
3. Kuleta Umoja wa Mwili wa Kristo. Pia aliongeza kuwa kamati ya
maandalizi imeandaa utaratibu wa mabasi kuanzia Akiba, Palm Beach na
Muhimbili ambapo yatafanya kazi kuanzia saa 1-3 usiku.
Habari na picha kwa hisani ya blog ya bukoba wadau
No comments:
Post a Comment