Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akikabidhi mchango wa sh. mil. 10 kwa Mchungaji George Fute ambaye ni
Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu Alex Malasusa wakati wa
hafla ya kuhitimisha harambee ya kuboresha usikivu wa Redio ya Dini ya
Upendo 107.7 FM yenye lengo la kuchangisha na kupata kiasi cha sh. Mil.
220 iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es
Salaam.
Mchungaji
George Fute ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu
Alex Malasusa akitoa shukrani kwa Mgeni wa Heshima katika hafla hiyo
ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa mara baada ya kukabidhi mchango wake pamoja na marafiki zake wa
sh. Mil. 10 kwa ajili ya kuboresha na kuongeza wigo mpana wa kusikika
kwa Redio ya Upendo FM.
Mheshimiwa Edward Lowasa mgeni maalum akisalimiana na Askofu mstaafu Elinaza Sendoro wa K.K.K.T |
Mh.
Lowassa akiongoza zoezi zima la uchangishaji wa fedha kwa watu mbali
mbali waliofika ukumbini hapo kw ajili ya kuichangia Redio Upendo FM.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa
hotuba yake fupi kabla ya kukabidhi mchango wake na kuongoza harambee
hiyo iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es
Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimpongeza Mwanamuziki wa Ijili kutoka nchini Kenya,Sarah K ambaye
alishirikiana nae katika zoezi la kuchangisha fedha hizo.
Mchungaji
George Fupe ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu
Alex Malasusa akizungumza machache kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Askofu
Mkuu ambaye hakuweza kufika kwenye hafla hiyo.
Meneja wa Redio Upendo FM,Agatha Lema akisoma hotuba katika hafla hiyo.
Meneja wa Redio Upendo FM,Agatha Lema akiikabidhi hotuba hiyo kwa Mgeni Rasmi.
Muimbaji wa Muziki wa Injili kutoka nchini Kenya,Sarah K akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
Muimbaji wa Muziki wa Injili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo,Faraja Ntaboba akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
Muimbaji wa Muziki wa Injili ,Jennifer Mgendi akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
Muimbaji wa Muziki wa Injili,Joshua Mlelwa akiimba moja ya nyimbo zake katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia waumini waliofika ukumbini hapo.
Kwaya Kutoka K.K.KT Azania Front |
Kwaya toka K.K.K.T Vetenary |
Vikundi vya Kwaya mbalimbali.
Bwana Lenard Shayo akiwa na wageni toka USA Jimbo la Michigan Nancy Buchkuski, Joan Patacony wakiwa na mdau Julieth Mutabiilwa |
Watu mbalimbali waliofika katika tamasha hilo picha kwa hisani ya michuzi blog |
Great!
ReplyDelete