Tamasha hili lilifunguliwa rasmi kwa maombi yaliyoongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo la Manzese,kisha kufuatiwa na uimbaji uliofunguliwa na kwaya ya Uinjilisti Sayuni Kinondoni na kuhitimishwa na kwaya ya Uinjilisti Manzese, Kilichowavutia watu zaidi ni jinsi ambavyo kwaya ya Uinjilisti Kawe ambao kila kukicha wamekuwa wakiongeza kiwango cha uimbaji,zamani kwaya hii ilikuwa imepewa jina la utani kwa kuitwa wanajeshi kutokana na waimbaji wake wengi kuwa wanajeshi kutokana na eneo walipo.Kisha kwaya ya Uinjilisti Kijito ambao watu walipendezwa na namna ya mpangilio wao wa muziki ulivyokuwa mzuri lakini pia na uchezaji wao. Sayuni hawakuwa nyuma wakiongozwa na soloist wao Balisidya aliyekonga nyoyo za watu jinsi alivyokuwa akicheza na sauti. Umoja huo wa kwaya za Uinjilisti na Uamsho(UKUU)umekuwaa ukifanya matamasha mara mbili kwa mwaka,mwezi wa tano kwa kuzigawanya kwaya katika makundi na tamasha la mwezi wa nane kwaya zote zaidi ya 15 zinakutana pamoja kwa uimbaji na kubadilishana vipawa.
BAADHI YA MATUKIO KATIKA PICHA
Waite Sayuni wazee wa Kinondoni ndio waliofungua tamasha |
Wazee wa nguo za asili ndo wenyewe
Wanamuziki wa Kwaya hiyo wakiwa wanavicheza vyombo vyao vya muziki
Kwaya ya Hananasifu wakiwa jukwaani ndani ya BnW (Black and White) |
Hawa ni Teule Mwananyamala ndio jina lao wakijishughulisha jukwaani |
Katika mtizamo mwingine walionekana hivi
Fundi Mitambo Lukio Mjema akiwa kwenye mixer akiweka mambo sawa
Modest Mogan akiongoza sifa wakati wa matoleo
Uinjilisti Kijito wakisebeneka kwenye jukwaa
Jopo la wanamuziki wa Kijito wakivipapasa vyombo vyao
Anaye lead wimbo ni Gerald John, mwite Big ndo nick name yake ama (the voice)
Allen Mwaipaja akilitumia gunzi vema
Mwana dada Violet Mshiu wa Revocatus
(aliyenyoosha kidole juu) akiimba kwa hisia
Shoto ni Eugene Mwamwembe akiwa na Kutyferra wakivicheza vinanda |
Uinjilisti Kawe on the stage
Mwalimu Elidadi akiwaweka sawa waimbe kwa ustadi kama walivyolitawala jukwaa
Kawe wakiwa smart stejini
Hatimaye Calvary Manzese wakafunga dimba,
Wanamuziki wa Manzese wakianzisha wimbo
Calvary Manzese kwa ujumla wao wakiwa kwenye steji
Washika magunzi wa Manzese wakifanya makamuzi
Nice event, God bless everyone who participated and those who posted these events. Amen
ReplyDeleteVale Kamugisha
Hongereni watumishi kwa kumuinua Kristo Yesu! Mungu awabariki sana na muendelee kumsifu Mungu wetu aliye hai!
ReplyDelete