MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, April 30, 2012

KKKT-DMP KIJITONYAMA WAZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Jana imezindua Jengo la ghorofa tisa lijulikanalo kwa jina la Kijitonyama Lutheran Centre sambamba na uzinduzi mwingine wa nyumba ya ghorofa moja ambayo usharika wa Kijitonya umeinunua nayo ikiitwa Kijitonyama Lutheran Centre Annex. Uzinduzi huo ulifanywa na Askofu mkuu wa Kanisa hilo Dr.Alex Gehaz Malasusa. Gharama za ujenzi wa jengo hilo kubwa na ununuzi wa nyumba hiyo umeligharimu kanisa hilo takribani shilingi za kitanzania bilioni 3.5 Jengo hilo litatumika kwa shughuli za kiofisi na nyingine kama zitakavyobainishwa na hapo baadae.
Katika uzinduzi huo ulioambatana na ibada askofu huyo aliwaasa wakristo kujitokeza kwa wingi katika kuchangia mchakato wa kupata katiba mpya. 
Fuatana nami kwa tukio hilo katika picha.

 Hilo ndilo jengo lililozinduliwa,Wanaoonekana kwenye picha ni wadau mbalimbali waliojihusisha katika kazi mbalimbali za kuhakikisha ujenzi hata uzinduzi unakwenda kama ulivyopangwa

 Huu ni upande wa kushoto wa jengo hilo

 Upande wa nyuma linaonekana hivi

 Maandamano yalioongozwa na kundi la wapiga tarumbeta, kuelekea kwenye jengo hilo kwa shughuli ya uzinduzi

 Watoto wa sunday school wa kanisa hilo nao wakiwa kwenye maandamano

 Wazee wa kanisa wakiwa na nyuso za furaha na wakiwa katika hali ya utanashati na kupendeza nao walihusika katika maandamano hayo.

 Parish wokers na watumishi wengine wa kanisa nao hawakuwa nyuma katika maandamano

 Wachungaji wa sharika mbalimbali nao wakiwa kwenye maandamano

 Na mwisho wa maandamano walikaa wakuu wa jimbo makatibu wa kuu pamoja na Askofu A.G. Malasusa

 Viongozi,waumini na vikundi vya kwaya wakiwa tayari wakisubiri uzinduzi wa jengo hilo

 Askofu Alex G. Malasusa akianza ibada ya uzinduzi wa jengo hilo

 Jopo la watumishi wa Mungu wakisikiliza kwa makini

 Kwa mbali ni kwaya aalikwa ya Winner toka Ubungo 

 Wazee wa kanisa nao wakiwa makini

 Parish wokers nao pia wakiwa katika hali ya uchaji

 Katibu wa baraza la wazee wa kanisa la Kijitonyama akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo

 Eng. Sanyiel Kishimbo aliyekuwa msimamizi wa ujenzi huo nae akitoa taarifa kabla ya kulikabidhi kwa katibu wa dayosisi

 Wakati ukafika na utepe ukakatwa tayari jengo likazinduliwa kelele za shangwe na vigelegele vikasikika

 Askofu akiwa amegusa lango kuu la jengo hilo huku akibariki kila aingiaye na kutoka katika mjengo huo

 Hii ni sehemu ya basement iliyomo ndani ya jengo hilo itakayotumika maalum kufundishia darasa la Sunday school kwa watoto wa kanisa hilo la Kijitonyama

 Watoto wakaonyesha furaha yao kwa kuimba wimbo wakifurahia sehemu ya ukumbi huo itakayotumika kama darasa kwao

 Hatua iliyofata ni ile ya kufungua sehemu ya jiwe la uzinduzi

 Askofu Malasusa akifungua sehemu ya jiwe la ufunguzi

 Jiwe la uzinduzi linaonekana hivi

 Hii ndiyo Kijitonyama Lutheran Centre Annex kabla ya kuzinduliwa

 Askofu Malasusa akizindua nyumba hiyo ya ghorofa moja kwa kukata utepe

 Watumishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wazee wa kanisa wakipozi katika picha ya pamoja

 Wachungaji wote waliokuwepo nao wakapozi katika picha ya pamoja

 Kwaya ya Winners toka Ubungo wakihudumu katika ibada

 Kwaya ya Umoja ya usharikani hapo wakihudumu katika ibada

 Askofu Malasusa akihubiri

 Hii ni kwaya ya uamsho, wakimwimbia Mungu wakati wa ibada

3 comments:

  1. Hongera sana WanaKijito, Mungu azidi kuwabariki sana. Ahsante kaka yangu kwa kutelea matukio haya ya Kijito, kwani unatusogeza na kutukumbusha mengi,Nimefurahi kuwaona watu weeeengi.

    Mungu awe nanyi daima ipo siku tutakuwa pamoja tena kwa uwezo wa Mungu.

    ReplyDelete
  2. Nilikuwa nazisubiri kwa hamu sana hizi picha. Hongereni sana. Sasa ni full kujiachiaaaa

    ReplyDelete
  3. God is great, blessings to us all, amen.

    ReplyDelete