Katika nyumba ya ibada ya Kijitonyama K.K.K.T Jana palikuwa hapatoshi kwa wingi wa neema zilizojaa kupitiliza katika vipindi vyote vya ibada. Ibada ambayo iliongozwa na Mch. Ernest Kadiva akishirikiana na mtheolojia pamoja na Mhubiri machachari huyu si mwingine bali Mwinjilisti Kayuni ambaye alihuburi habari za Roho Mtakatifu. Kwani jana kanisa hilo lilikuwa linakumbuka siku ya Pentekoste. Pamoja na Kikundi cha sifa yaani Praise Team zilikuwepo kwaya nyingine pia Ikiwa ni Uinjilisti Kijito pamoja na Kwaya Kuu ya Usharika. Mambo hayakuwa haba. Angalia matukio hayo katika picha.
Kijana Allen Mwaipaja akiongoza Praise Team katika kusifu na kuabudu
Kanisa wakiwa katika hali ya kumsifu Mungu
Kwaya ya Uinjilisti wakimsifu Mungu
Kwa mbali anaonekana mamaNancy Buchkuski na rafiki yake Joan Pataconi na mzee Leonard Shayo wakicheza Ndani ya Safina.
Mambo ya Kantate Domino tumwimbie Mungu kwa makabila yote, Jana ilikuwa siku ya Wahaya kumwimbia Mungu kwa lugha yao.
Katibu wa Barala la wazee Kijitonyama mama Victoria Kisyombe akiwatambulisha wageni toka Usharika rafiki wa Kijitonyama, Unaoitwa Our Saviours Lutheran Church. Aliye katikati ni mama Nancy Buchcuski akiwa na rafiki yake Joan Pataconi wamekuja kuwatembelea jamaa na marafiki.
Katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee wa kanisa, wakipokea zawadi mbalimbali walizotoa wageni hao
Mwinjilisti Kayuni akihubiri kwa msisitizo
Kwaya Kuu waliokuwepo jana, wakisikiliza kwa makini wakati ibada ndo inaelekea ukingoni
Mtumishi ubarikiwe sana! Ibada ya jana (27/05/2012), ilikuwa ya kipekee kwa kweli; kuanzia uchaji, mahubiri na hata uimbaji! Roho mtakatifu aendelee kutupigania na kutufundisha jinsi ya kuenenda ili shetani asiweze kutufarakanisha wana wa KIJITO!
ReplyDeleteAhsante sana kaka kazi nzuri sana,Pamoja daima
ReplyDelete