Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Suleiman Kova alisema mtoto mmoja (mkristu jina tunalo) akiwa
katika michezo na mwenzake wa Kiislamu walianza kubishana, kuwa endapo
ukikojolea kitabu cha dini ya Kiislamu (msaafu) lazima ugeuke kuwa
kichaa, hivyo Josephat alibisha na kumwambia mwenzake anaweza kufanya
hivyo na kutodhurika.
Baada ya mabishano hayo Josephat aliamua kukikojolea kile kitabu ili
aone kama angelidhurika kama alivyoelezwa na mwenzake, lakini haikuwa
hivyo. Hata hivyo baadaye yule wa kiislamu alitoa taarifa kwa wazazi
wake ndipo yalianza mazungumzo kati ya wazazi kwa wazazi.
Kova alisema mvutano huo ulifika katika kituo kidogo cha polisi na
ndipo baadhi ya Waislamu walianza kujitokeza na kutaka wapewe maelezo na
kadri ya walivyoongezeka eneo la kituo hali ilianza kuwa mbaya kwani
baadhi yao walionekana kutaka kufanya fujo na kuomba wapewe yule mtoto
ili wamuadhibu.
Baada ya hali kuwa tete Jeshi la Polisi lilileta askari wa kutuliza
ghasia FFU kuwataka waliokuwa kituoni kuondoka kwa amani lakini baadhi
yao walipinga hivyo kuanza kutumia nguvu kuwatawanya. “Baada ya wananchi
hao kutawanyishwa baadhi walijikusanya na kuzunguka huku wakifanya fujo
kwa kushambulia Makanisa, Makanisa yalioshambuliwa ambayo yote ni ya maeneo ya Mbagala Kizuiani ni
pamoja na Kanisa la Anglikana, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT-Mbagala) na Kanisa la Sabato ambayo yamevunjwa vioo pamoja na
kuharibu mali kama magari yaliyokuwa yameegeshwa eneo la kanisa na
mengine waliokutana nao waandamanaji hao.na mali za watu,” alisema Kova akizungumza na
chombo kimoja cha habari.
K.K.K.T Mbagala ambalo ndilo lilioharibiwa
Mlango wa kanisa ukiwa umevunjwa vioo
Akina mama wenye mzigo wa maombi, wakiomba Mungu awarehemu waliofanya uharibifu huo
Vyombo mbalimbali vya kanisa hilo vilivyochomwa moto
Watu mbalimbali waliofika kanisani hapo kujionea uharibifu uliotokea
Gari la Mchungaji wa usharika hou wa Mbagala likiwa limeharibiwa vibaya
Jionee uharibifu uliofanywa
Kushoto unaonekana msikiti walipotokea waumini wa dini ya kiislamu kwenda kufanya uharibifu huo.
Dean Geoge Fupe msaidizi wa Askofu mkuu wa kanisa la K.K.K.T Alipofika kanisani hapo kuona kulichojiri
Viti vikiwa vimerushwa huku na kule
Mimbari ya kuhubiria inavyoonekana baada ya kuchomwa moto
Mlango wa kanisa hilo na vitu mbalimbali vikiwa katika hali ya kusikitisha
Ofisi ya Mchungaji ilionekana hivi baada ya kutiwa moto
Inasikitisha sana
Mchungaji George Fupe akizungumza na mchungaji wa Mbagala juu ya yaliyojiri
No comments:
Post a Comment