MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, October 8, 2012

Anglican Kurasini Wahitimisha Mkutano wa Kiroho

Kanisa Anglican lilipo Kurasini karibu kabisa na studio za WAPO Radio, Jana walihitimisha mkutano mkubwa wa injili ulichukua takriban siku nane. Mkutano ulihudumiwa na watumishi mbalimbali wa Mungu akiwemo Mwinjilisti Mgogo toka Mbeya. Katika kuhakiki injili inawafikia wakazi wa maeneo yao huku watu wakimsifu na kumwabudu Mungu vyema jana siku ya kuhitimisha walialika kwaya ya Uinjilisti toka Kijitonyama. Ambao walihudumu tangu kwenye ibada asubuhi na baadae kwenye mkutano jioni yake. Na haya ndiyo yaliyojiri

 Kwaya ya Uinjilisti Kijito on the stage wakisebeneka ki-gospel zaidi

 Sifa ikishaanza ni vigumu mno kubaki umesimama bila kumchezea Mungu wako, vinginevyo unakuwa hujatambua ni wapi Mungu kakutoa

 Ni wakati wa Praise and Worship watu wakijimimina mbele za Bwana kwa shangwe

 Kwaya ya Nazareth wakitumika kwa uimbaji madhabahuni

 Kwaya ya Nazareth wakiwa stejini katika mkutano wa kirohi uliofanyika nje kidogo ya kanisa lao

 Umati wa watu waliofika viwanja vya kanisa la Anglican Kurasini kusikiliza neno la Mungu
Kwaya ya uinjilisti Kijito wakiungurumisha  sifa on the stage.

No comments:

Post a Comment