Kanisa la A.I.C.T Dar es Salaam, Pastorate ya Tabata mtaa wa Kilungule jana limefanya Harambee kubwa ya Ujenzi wa kituo cha watoto, umaliziaji wa jengo la ibada na uchimbaji wa kisima cha maji kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo. Katika ibada iliyoambatana na harambee Askofu mkuu wa kanisa hilo Charles Salala alisisitiza kuwa jamii inapaswa kuwajali watoto na kuwa na hofu ya Mungu.
Mh. William Mganga Ngeleja (MB) Ndiye aliyeongoza harambee hiyo iliyokuwa na mafanikio nakujikuta wakusanya takribani milioni za kitanzania Hamsini. Pia katika ibada hiyo zilialikwa kwaya mbalimbali za kanisa hilo ikiwa ni pamoja na zile za nje ya kanisa hilo.
Haya ndiyo yaliyojiri katika picha
Jengo la ibada mtaa wa Kilungule linavyoonekana kwa sasa
Kwaya ya mtaa wa Kilungule wakimsifu Mungu katika ibada hiyo
Dar es Salaama Choir ya Pastorate ya Magomeni wakiwajibika
Ujumbe kwaya nao walikuwepo, hii ni kwaya ya akina mama peke yao
CVC Chan'gombe Vijana Choir wakiliteka jukwaa
Mass Choir wakisifu na kuabudu katika ibada hiyo.
Kwaya alikwa toka K.K.K.T Kijitonyama walikuwepo pia
Umati wa watu waliofika katika ibada hiyo wakisikiliza kwa makini
Mchungaji wa A.I.C.T Pastorate ya Tabata akisisitiza jambo mbele ya waamini
Askofu Charles Salala akihubiri mbele ya waamini
Jopo la wageni waalikwa waliofika katika ibada hiyo, tokea shoto ni mgeni aliyeambatana na mgeni rasmi akifuatiwa na Mr. Paul Luchemba, Mh. William Ngeleja akiwa na mkewe Brandina
Mr. Paul Luchemba ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee, akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi
Mgeni rasmi Wiliam Ngeleja (MB) akijibu risala ya waamini
Wanakamati wakiwa tayari kabisa kuanza mnada katika harambee
Mbuzi wakisubiri kunadiwa
Kuku wakiwa wamepata lifti kwenye spika, walipata pumziko huku wakisikiliza neno la Mungu kwa karibu na bila bugdha yeyote.
No comments:
Post a Comment