Katika uzinduzi huo ambao umehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo askofu wa kanisa hilo la AICT dayosisi ya Shinyanga,na wachungaji, pamoja na kwaya mbalimbali zikiwemo AIC Dar es salaam Choir kutoka Magomeni, Ukombozi Choir kutoka K.K.K.T Msasani, Majestic Singers kutoka E.A.G.T City centre, Neema Gospel Choir kutoka AIC Chang'ombe pamoja na Matendo Choir ya AIC Chang'ombe.
Matukio Katika Picha
Kama linavyoonekana hapo juu, Ni jengo la kitega uchumi la kwaya ya CVC litakapokuwa limekamilika
Matendo Kwaya ya A.I.C.T Changombe
Mafundi mitambo wakiwa busy kuhakiki muziki unawafikia vilivyo wasikilizaji
Mpiga picha za video wa CVC akiwa kazini
Majestic Singers wakiwa wameketi kwa utulivu wakisikiliza yanayojri
Neema Gospel Choir ya A.I.C.T Changombe wakilikamata jukwaa
Huyu bwana mdogo wa kwaya ya Neema Gospel Choir ya A.I.C.T Changombe alikonga nyoyo za watu kwa ustadi aliokuwa akiutumia kucheza
Dar es Salaam Kwaya ya A.I.C.T Magomeni wakiwa busy jukwaani
Majestic Singers toka E.A.G.T City Centre a.k.a Wazee wa kuotesha nyama kwenye mifupa
wakimtukuza Mungu jukwaani
Nyomi lililofika kuona nini kinaendelea
Kamati ya maandalizi wakiweka mambo sawa kabila ya uzinduzi
Meza kuu walipokaa wangeni rasmi, Tokea kushoto ni askofu wa A.I.C.T Dayosisi ya Shinyanga akifatiwa na Mh. William Ngeleja (MB) na mgeni aliyemsindikiza
CVC Haoo wakiingia jukwaani kwa style ya pekee wanakimbia kwa shangwe na vigelegele kuelekea jukwaani tayari kuizindua Album yao
CVC Wakionesha namna jengo lao litakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika
Wana CVC tayari tayari kwa kuimba
wakisikiliza risala inayosomwa na mwenyekiti wa kwaya yao
Mwenyekiti akisoma risala kwa mgeni rasmi
Picha ya jengo hii hapa
Mheshimiwa Ngeleja akijibu risala ya wana CVC
Kwaya mbalimbali wakiwa wameketi wakisikiliza yanayojiri
Askofu wa A.I.C.T Dayosisi ya Shinyanga akitoa maneno ya hekima
Mheshimiwa William Ngeleja akizindua rasmi DVD ya USIKU WA MANANE kwa kukata utepe
Jopo la wageni wazito wazito walioambatana na mgeni rasmi wakiwa tayari kusema yaliyoko mioyoni mwao katika kuchangia uzinduzi huo
MC Machachari Bw. Tito akiweka DVDs tayari kwa mnada
Mheshimiwa Ngeleja akiwakaribisha wageni alioambatana nao kuanza kutamka pledges zao
Mch. Charles Mzinga toka K.K.K.T Azania Front ni mmoja wa wachungaji waliokaribishwa katika uzinduzi huo
Askofu toka Dayosisi ya Shinyanga ya kanisa hilo akisikiliza kwa makini
Wageni toka nchi jirani ya Kenya nao wakimtolea Mungu
Wageni rasmi wakizawadiwa DVD za USIKU WA MANANE |