MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, September 27, 2011

Jacob na Martha Waingia Kwenye Chama

Juzi kati tarehe 24 Septemba 2011, Jacob Absalom wa Mwaipaja aliamua kuvunja ukimya kwa Martha Abraham wa Lubwaza  pale alipokiri adharani mbele ya watu lukuki na kujikuta akisema "I DO" kutokea moyoni mwake bila ya shinikizo la mtu yeyote ndivyo alivyofanya Martha kwa Jacob pia. Ikawa ni siku ya furaha kwa watu wote waliofika K.K.K.T Kijitonyama kwenye ibada ya ndoa na waliofika katika ukumbi wa Sunset Halls (Flamingo) Mbezi ya Africana jijini Dar es Salaam, Kwa wewe ambaye hukuweza kufika ambatana nami katika picha hizi.

Monday, September 19, 2011

KKKT Kijtonyama Jana Jumapili walifanya ibada maalum iliyokwenda sambamba na Harambee ya kuchangia jengo la Kitega uchumi litakalojulikana kama Kijitonyama Lutheran Centre.Ibada hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa kanisa hilo Tanzania. Askofu Alex Gehaz Malasusa akishirikiana na wachungaji Charles Mzinga, Hoyce Mbowe na Ernest Kadiva.  Malengo yao yakiwa ni kukusanya Tsh Milioni mia mbili na nusu.
Fuatana nami katika matukio kwa njia ya picha.

Kama linavyoonekana hili ndilo jengo la Kijitonyama Lutheran Centre ambalo litaanza kutumika hivi karibuni baada ya kukamilika ujenzi wake.
Kama linavyoonekana bango lililokuwa ndani ya kanisa likionesha ujumbe na lengo la kuchangia gharama za umaliziaji wa jengo hilo la KLC
Mheshimiwa Baba Askofu Alex Gehaz Malasusa ambaye ndiye aliongoza ibada nzima na kuwahamasisha washarika jinsi ya kubarikiwa wanapomtolea Mungu mali zao.

Pichani baba Askofu (mwenye joho la kijani) Akiwa na wachungaji. Wa kwanza kushoto ni Mch. Charles Mzinga, watatu ni Mch. Hoyce Mbowe na wa nne ni Mchungaji Ernest Kadiva. Mchungaji Charles na Hoyce wamewahi kuwa wachungaji wa usharika wa Kijitonyama pia

Moja ya kwaya iliyohudumu katika ibada hiyo ilikuwa ni hii ya Vijana Usharika wa Kijitonyama

Katibu wa baraza Dr. Victoria Kisyombe akisoma risala kwa mgeni rasmi baba Askofu Alex Malasusa

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi akizungumza jambo kabla ya kuanza rasmi kwa harambee hiyo

Ndugu Hans Macha akizungumza mbele ya usharika kile ambacho atamtolea Mungu

Mr. Lenard Shayo nae hakusita kutoa lililokuwa moyoni mwake katika kumtolea Mungu

Mama Esther Maro kwa furaha kabisa akitamka ni nini atakachomtolea Mungu.

Mmoja wa wazee wa kanisa akitamka sadaka yake

Mr. Bosco Gadi naye pia kwa ujasiri akisema mbele ya Askofu nini atamtolea Mungu kuchangia K.L.C

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akinadi Bed Cover katika kufanikisha harambee hiyo

Mmmoja wa washarika alinunua picha hii kwa furaha kubwa, lengo likuwa ni kuchangia K.L.C

Familia hii ilimtolea Mungu kwa kununua picha hii. Kama wanavyoonekana wenye furaha.

Bwana Benson Mahenya na Familia yake walimtolea Mungu sadaka yao kwa unyenyekevu kama wanavyoonekana kwenye picha.
Baadhi ya vitu vilivyoletwa na washarika kwaajili ya kunadiwa, kulia ni benchi la ufundi lililokuwa likishughulika na ukusanyaji wa kumbukumbu

Nipeni bei..... Alisikika mzee huyu akinadi blanketi

Baiskeli hii yenye injini pia ilinadiwa na kufanikisha kiwango kizuri katika kuchangia K.L.C

Wadau wengine waliokuwepo katika benchi la ufundi la kukusanya kumbukumbu

Friday, September 2, 2011

Atughanile Awakawaka Katika Sendoff Yake

 Ijumaa ya Tarehe 15 Julai Mdau, Atughanile Mwasomola aling'ara katika Sendoff yake. Iliyofanyika mji kasoro bahari. Huku akisindikizwa na wadau wenzie toka Dar.

 Hapa akiingia ukumbini na wadau wa kwaya yake wakimsindikiza

 Akiwa na mpambe wake baada ya kuingia ukumbini.

 Akienda kumtafuta my husband wake mtarajiwa, huku akiwa na zawadi mkononi

Baada kumwona my husband wake mtarajiwa akampeleka mbele ya hadhara. Kama wanavyoonekana kila mtu na mpambe wake
Akikata keki
 Akimlisha mpambe keki mpambe wake 

 Kwa adabu kabisa akimpa shangazi zawadi kwa malezi mema

 Mtarajiwa akiwa amepozi na baba na mama yake

 Picha ya familia

 Wanakwaya wenzake waliokuwepo katika send off ya Atughanile wakifurahi pamoja naye on the stage!
 Wadau wakaona si vema kuondoka hivi hivi wakadondosha accapela moja la ukweli

 Hao na jizawadi kuuuuubwa wakienda kumpongeza mwenzao


Wadau wakaamua kupiga picha ya pamoja kwa ukumbusho, na alama ya kwamba walifika katika send off ya mwenzao Atughanile