KKKT Kijtonyama Jana Jumapili walifanya ibada maalum iliyokwenda sambamba na Harambee ya kuchangia jengo la Kitega uchumi litakalojulikana kama Kijitonyama Lutheran Centre.Ibada hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa kanisa hilo Tanzania. Askofu Alex Gehaz Malasusa akishirikiana na wachungaji Charles Mzinga, Hoyce Mbowe na Ernest Kadiva. Malengo yao yakiwa ni kukusanya Tsh Milioni mia mbili na nusu.
Fuatana nami katika matukio kwa njia ya picha.
Kama linavyoonekana hili ndilo jengo la Kijitonyama Lutheran Centre ambalo litaanza kutumika hivi karibuni baada ya kukamilika ujenzi wake.
Kama linavyoonekana bango lililokuwa ndani ya kanisa likionesha ujumbe na lengo la kuchangia gharama za umaliziaji wa jengo hilo la KLC
Mheshimiwa Baba Askofu Alex Gehaz Malasusa ambaye ndiye aliongoza ibada nzima na kuwahamasisha washarika jinsi ya kubarikiwa wanapomtolea Mungu mali zao.
Pichani baba Askofu (mwenye joho la kijani) Akiwa na wachungaji. Wa kwanza kushoto ni Mch. Charles Mzinga, watatu ni Mch. Hoyce Mbowe na wa nne ni Mchungaji Ernest Kadiva. Mchungaji Charles na Hoyce wamewahi kuwa wachungaji wa usharika wa Kijitonyama pia
Moja ya kwaya iliyohudumu katika ibada hiyo ilikuwa ni hii ya Vijana Usharika wa Kijitonyama
Katibu wa baraza Dr. Victoria Kisyombe akisoma risala kwa mgeni rasmi baba Askofu Alex Malasusa
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi akizungumza jambo kabla ya kuanza rasmi kwa harambee hiyo
Ndugu Hans Macha akizungumza mbele ya usharika kile ambacho atamtolea Mungu
Mr. Lenard Shayo nae hakusita kutoa lililokuwa moyoni mwake katika kumtolea Mungu
Mama Esther Maro kwa furaha kabisa akitamka ni nini atakachomtolea Mungu.
Mmoja wa wazee wa kanisa akitamka sadaka yake
Mr. Bosco Gadi naye pia kwa ujasiri akisema mbele ya Askofu nini atamtolea Mungu kuchangia K.L.C
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akinadi Bed Cover katika kufanikisha harambee hiyo
Mmmoja wa washarika alinunua picha hii kwa furaha kubwa, lengo likuwa ni kuchangia K.L.C
Familia hii ilimtolea Mungu kwa kununua picha hii. Kama wanavyoonekana wenye furaha.
Bwana Benson Mahenya na Familia yake walimtolea Mungu sadaka yao kwa unyenyekevu kama wanavyoonekana kwenye picha.
Baadhi ya vitu vilivyoletwa na washarika kwaajili ya kunadiwa, kulia ni benchi la ufundi lililokuwa likishughulika na ukusanyaji wa kumbukumbu
Nipeni bei..... Alisikika mzee huyu akinadi blanketi
Baiskeli hii yenye injini pia ilinadiwa na kufanikisha kiwango kizuri katika kuchangia K.L.C
Wadau wengine waliokuwepo katika benchi la ufundi la kukusanya kumbukumbu
No comments:
Post a Comment