Jumapili ya wiki iliyopita ilikuwa ya baraka sana kwa Usharika wa Kijito.
Pamoja na kuwa na ibada nzuri iliyojaa ratiba nyingi.
Kwaya kuu ya usharika ilipata nafasi ya kuzindua album yao mpya
Mgeni rasmi wa shughuli hiyo alikuwa mh. Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu.
Pia baadae jioni
kulikuwa na tamasha la uimbaji uliozishirikisha kwaya za uinjilisti na uamsho jimbo la kaskazini (UKUU)
Fuatana nami katika matukio kwa njia ya picha
Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akikata utepe
ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Album hiyo.
Kikosi kazi cha kwaya ya Uinjilisti Kijito
wakiwa tayari kwa kupanda jukwaani.
Washika magunzi nao hawakuwa nyuma
katika kupaza sauti zao kumsifu Bwana Yesu
Kwa shangwe na furaha vijana wakipanda jukwaani kwa tabasamu
kuubwa kabisa wakionyesha raha ktk Kristo
Kama uonavyo wakilipamba jukwaa. Kweli ipo raha katika kumtumikia Mungu
Wakiwa wametulia tayari kwa kuanza uimbaji
Akionekana kwa mbali kijana Israel Mujumba akiliongoza
kundi katika wimbo wa Nakimbilia msalabani.
Pendo Mwambungu a.k.a binti wa kuimba key za juu
akiliongoza kundi kwa hisia za hali ya juu
Wanamuziki nao wakipiga vyombo kwa ustadi mkubwa.
Tokea shoto ni Dr. Tuntufye akipiga bass guitar,
Enock akiwa na rhythm, Micah Songo akilipiga solo
na Kuttyfera akibofya kinanda
Ni uimbaji kwa kwenda mbele
Kwaya ya Uinjilisti Ubungo
Uamsho Kijito wakilipamba Jukwaa
Wazee wa kazi Sayuni kinondoni nao walikuwepo
Wapiga vyombo wa kwaya ya Sayuni wakiwa kazini
Mpiga kinanda wa Kwaya ya Uinjilisti Sayuni nae akionesha ustadi wake
Drummer Boy wa Sayuni akionesha Umahiri wake
Kwa kuangalia vazi tu utawajua hawa ni Sayuni wazee wa Kinondoni
Wakizipaza sauti zao ndani ya vazi la kimasai, Ilikuwa raha sana
Foma Foma akiwa na Drummer Boy wa Sayuni katika pozi