Wapenzi wa Blog hii. Naomba radhi kwa kuwacheleweshea matukio ya wiki iliyopita.
Ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Nimewaletea matukio kwa njia ya
video na matukio kwa njia ya picha yakuwa hewani muda si mrefu.
Yafuatayo ni matukio kwa njia ya video Utaona watoto wa Kijitonyama Sunday School
walivyoonesha kwa washarika jinsi walivyokuwa wamejiandaa kwenda katika tamasha la watoto lililofanyika jumapili iliyopita tarehe 5 June katika usharika wa Magomeni Mviringo. Pia utaona moja ya kwaya iliyohudumu kwenye ibada ya siku hiyo. Nayo si nyingine ni kwaya ya Uinjilisti ya usharika huo. Wakiimba wimbo wa nakimbilia msalabani.
Hivi ndivyo linavyonekana K.K.K.T Kijito
Hivi ndivyo watoto wa Sunday School ya Kijito walivyoonesha vipaji vyao
Mchungaji Kadiva akisema neno baada ya watoto kuimba
Hatimaye waliombewa baraka ili wakauwakilishe vyema usharika
Mdau Phesto Mwakyusa toka Ughaibuni akikabidhi zawadi kwa usharika toka ufini.
Bwana Lenard Shayo alikuwepo kuzipokea akisaidiana ma mchungaji wa usharika
Kwaya kuu ya usharika nao walikuwepo ndani ya nyumba
Kwaya ya Uinjilisti wakihudumu ibadani siku hiyo
Kwaya ya Uinjilisti wakiwa katika mtizamo mwingine
Nakimbilia Msalabani
Nakimbilia Msalabani
Mchungaji akisema jambo fulani kuhusu wadau hao. kama picha inavyosema
Ndo ibado inaishiaishia hivyo
Shoto ni Mwalimu Kisasa mtaalam na mwongoza uimbaji wa nyimbo hapo usharikani
Mambo hayakuwa haba siku hiyo kijana Aggrey alipoamua kufunga ndoa
Tabasamu la ukweli linaonekana jamani
Anatafakari tu raha aliyonayo moyoni hakuna ajuaye ila yeye tu!
Step by step akiuelekea mlango wa kanisa tayari kwa ibada ya kufunga ndoa
Asante kaka kwakutukumbusha haya!! Mchungaji mama Mbowe yuko usharika gani sasa hivi na Mchungaji Hiza jee?. nimekumbuka nyumbani.
ReplyDelete