Dk Mponda alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua matumizi ya Bajaji kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa. Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumzuia mchungaji huyo kuendelea na utoaji wa dawa mpaka serikali itakapojiridhisha na hali ya usalama pamoja na uwezo wa dawa hiyo.
“Kutokana na hali halisi ya usalama wa kiafya kwa sasa katika eneo hilo, kuna hatari ya kuwepo kwa milipuko ya magonjwa kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka,” alisema Dk Mponda.
kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Foleni kuelekea kwa Mchungaji Mwasapile
Dawa ikichemshwa
Dawa iliyochemshwa tayari kwa kunywa
Mchungaji Mwasapile akitoa dose
Watu mbalimbali waliofika kijijini huko
Mapumziko baada ya kupata dawa
Hii naikubali,Mungu asaidie tu iwe inaponya kweli maana watu wamechoka kujisika nafuu wanataka kupona!
ReplyDelete