MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, November 18, 2010

Kwaya ya Uinjilisti Kijito Ziarani Mtaa wa Ununio

Jumapili iliyopita ya tarehe 14 Novemba. Kwaya ya uinjilisti ilipata kuhudumu katika mtaa mpya wa Ununio mtaa unaotunzwa na Usharika wa Boko. Wakiwa katika huduma ya kumtangaza kristo katika mtaa huo ambapo siku hiyo walikuwepo na viongozi wa kanisa akiwemo mkuu wa jimbo la kaskazini. Mchungaji Antha Muro na Askofu Gehazi Malasusa.
Lengo kuu lilikuwa kuuzindua jengo la ibada na harambee ya kuchangia umaliziaji wa jengo hilo. Makusudio yao ilikuwa kufikisha milioni 30. Kupitia "pledges" na vitu vilivyoletwa kunadiwa.

Angalia matukio kwa ufupi katika picha.
Hivi ndivyo linavyoonekana jengo la kanisa la mtaa wa Ununio! (ubavuni)

Hivi ndivyo linavyoonekana jengo la kanisa la mtaa wa Ununio! (Mbele)

Wakati Askofu Malasusa alipowasili mtaani hapo tayari kabisa kuianza ibada

Akielekezwa na mwenyeji wake (aliyemtangulia) Mchungaji wa usharika wa Boko.
Anayeonekana nyuma ni mchungaji Anta Muro Mchungaji na mkuu wa jimbo la kaskazini

Hawa ni baadhi ya wanakwaya wa kwaya ya uinjilisti kijito waliokuwepo.

Toka shoto ni Rosemary, Gift na Jacob nao walikuwepo, ni miongoni mwa wanakwaya
wa kwaya ya uinjilisti Kijito

Askofu akisisitiza jambo wakati wa mahubiri siku hiyo.

Bwana Aminiel Mushi akiwa katika kazi ya kunadi bidhaa mbali mbali zilizokuwepo

Kwa msisitizo akinadi Bw. Mushi

Akiifunga ibada ya siku hiyo na kutoa baraka kama anavyoonekana Askofu Malasusa
akiwa na watumishi wenzake. Akiwemo Mchungaji wa Usharika wa Kawe (Kulia)

Askofu malasusa akipozi kwenye picha

Hii ni picha ya pamoja askofu aliomba kupiga na washarika wote wa mtaa wa ununio!

No comments:

Post a Comment