MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, November 22, 2010

Kwaya ya Uinjilisti Kijito Yafanya Maandalizi ya Uzinduzi

Jumapili ya jana tarehe 21 Oktoba 2010, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ilifanya maandalizi ya uzinduzi wa Album yao mpya Ijulikanayo kama NDANI YA SAFINA. Walivaa T-shirts zenye rangi na majina mbali mbali ya album walizowahi kuzitoa. Ikiwa ni pamoja na Hakuna Mwanaume Kama Yesu, Hakuna Mungu Kama Wewe, Twaokolewa kwa Neema na Ndani ya Safina. Kwa habari zilizopatikana toka kwaya hiyo. Wanategemea kuzindua album yao hiyo tarehe 28 ya mwezi huu yaani jumapili ijayo. Uzinduzi huo utafanyika katika kanisa la KKKT Kijitonyama katika ibada zote mbili. Na baadae mchana watakuwa na tamasha la uimbaji.

Haya ni matukio baadhi katika Picha










No comments:

Post a Comment