MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, November 3, 2010

Harusi Ya Emma na Stella

Nimepata malalamiko toka kwa wapenzi wa blog hii wakitaka waone japo picha za harusi ya Emma na Stella ilivyokuwa. Nami sikufanya kusudi nikaingia mtaani japo kusaka chache. Hebu na tuziangalie wote!!!


Wapambe wa kike walionekana hivi jamani. Walipendeza sana!

Wakati wakiingia kanisani kwa mwendo wa madaha!

Kijana anasema kimoyomoyo leo ni leo jamani. Mungu ameniona!

Furaha inapoongezeka Dada Stella Aamini amini kama ni kweli ndo
siku ya harusi yake!

Pale lilipotoka tamko kwa mchungaji akisema. Ni nani anamtoa Stella kwenda
kwa Emmanuel? Baba wa watu kwa upole ikabidi ajitose kutamka neno!

Kijana alipokabidhiwa kifaa wacha furaha imjae kama vile kashukiwa na roho
mtakatifu siku ya pentekoste. Ilikuwa kidogo tu aanze kunena kwa Kisambaa!

Ni kama wanasema... Tulimaanisha ngoja tuwaoneshe kweli tulidhamiria.

Baraka naziwe juu yenu mnapoyaanza maisha mapya ya ndoa. Vijana
wakakomba mibaraka kibao toka madhabahuni! Ikawafurika mpaka myoni!

Hapa sisemi.... Angalia mwenyewe!!!

Punde tu Emma akapata ajira ya ulinzi........
anaangalia kushoto na kulia kama usalama upo maana ameshamiliki
so lazima ahakikishe usalama upo na amlinde!


Jamani si mnaona wenyewe? Wametimiza ndoto yao. Hebu njooni wapongezeni

Hongereni sana, mmetutia moyo wazee wenu! Tunawatakia maisha mema!

Mashosti nao wamo kupamba msafara!

Hapa wanatoka kanisani kwa furaha nyingi!

Tarumbeta walikuwepo kushughulisha shughuli ikaenda uzuuuuuri kabisa!

Sauti ndogo inatoka.... Hivi Stella unajua nakupenda mke wangu? Nae anajibu
huju ameinamisha kichwa. Mmmmmh! najua sinimeona?

WAMEPENDEZA HAWAJAPENDEZA?

No comments:

Post a Comment