MESSAGE
MESSAGE
Pages
Wednesday, December 1, 2010
Monday, November 22, 2010
Kwaya ya Uinjilisti Kijito Yafanya Maandalizi ya Uzinduzi
Jumapili ya jana tarehe 21 Oktoba 2010, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ilifanya maandalizi ya uzinduzi wa Album yao mpya Ijulikanayo kama NDANI YA SAFINA. Walivaa T-shirts zenye rangi na majina mbali mbali ya album walizowahi kuzitoa. Ikiwa ni pamoja na Hakuna Mwanaume Kama Yesu, Hakuna Mungu Kama Wewe, Twaokolewa kwa Neema na Ndani ya Safina. Kwa habari zilizopatikana toka kwaya hiyo. Wanategemea kuzindua album yao hiyo tarehe 28 ya mwezi huu yaani jumapili ijayo. Uzinduzi huo utafanyika katika kanisa la KKKT Kijitonyama katika ibada zote mbili. Na baadae mchana watakuwa na tamasha la uimbaji.
Haya ni matukio baadhi katika Picha
Haya ni matukio baadhi katika Picha
Thursday, November 18, 2010
Kwaya ya Uinjilisti Kijito Ziarani Mtaa wa Ununio
Jumapili iliyopita ya tarehe 14 Novemba. Kwaya ya uinjilisti ilipata kuhudumu katika mtaa mpya wa Ununio mtaa unaotunzwa na Usharika wa Boko. Wakiwa katika huduma ya kumtangaza kristo katika mtaa huo ambapo siku hiyo walikuwepo na viongozi wa kanisa akiwemo mkuu wa jimbo la kaskazini. Mchungaji Antha Muro na Askofu Gehazi Malasusa.
Lengo kuu lilikuwa kuuzindua jengo la ibada na harambee ya kuchangia umaliziaji wa jengo hilo. Makusudio yao ilikuwa kufikisha milioni 30. Kupitia "pledges" na vitu vilivyoletwa kunadiwa.
Angalia matukio kwa ufupi katika picha.

Akielekezwa na mwenyeji wake (aliyemtangulia) Mchungaji wa usharika wa Boko.
Anayeonekana nyuma ni mchungaji Anta Muro Mchungaji na mkuu wa jimbo la kaskazini
Anayeonekana nyuma ni mchungaji Anta Muro Mchungaji na mkuu wa jimbo la kaskazini
Toka shoto ni Rosemary, Gift na Jacob nao walikuwepo, ni miongoni mwa wanakwaya
wa kwaya ya uinjilisti Kijito
wa kwaya ya uinjilisti Kijito
Monday, November 8, 2010
Vijana wa Usharika Waweka Mikakati ya Kujikwamua
Jana jioni vijana wa KKKT usharika wa Kijitonyama, Walipata muda wa kukaa na kuzungumza mambo mbali mbali yahusuyo mambo yao. Miongoni mwa mikakati waliyonayo. Ni kuhakikisha kila kijana wa kanisa anamjua Mungu. Lakini pia kushiriki katika mambo mbalimbali ya jamii ikiwa ni pamoja na michezo, Kujifunza vyombo mbalimbali vya muziki. Na mengine mengi ikiwa ni pamoja na mipango ya kujikwamua kiuchumi. Kwa kuanzia vijana wameanza kwa kujisajiri kupitia fomu, simu ya mkononi, Pia kwa internet ambapo website itatoka hivi karibuni.
Fuatana nami uone matukio katika picha
Fuatana nami uone matukio katika picha
Wednesday, November 3, 2010
Harusi Ya Emma na Stella
Nimepata malalamiko toka kwa wapenzi wa blog hii wakitaka waone japo picha za harusi ya Emma na Stella ilivyokuwa. Nami sikufanya kusudi nikaingia mtaani japo kusaka chache. Hebu na tuziangalie wote!!!
Pale lilipotoka tamko kwa mchungaji akisema. Ni nani anamtoa Stella kwenda
kwa Emmanuel? Baba wa watu kwa upole ikabidi ajitose kutamka neno!
kwa Emmanuel? Baba wa watu kwa upole ikabidi ajitose kutamka neno!
Kijana alipokabidhiwa kifaa wacha furaha imjae kama vile kashukiwa na roho
mtakatifu siku ya pentekoste. Ilikuwa kidogo tu aanze kunena kwa Kisambaa!
mtakatifu siku ya pentekoste. Ilikuwa kidogo tu aanze kunena kwa Kisambaa!
Baraka naziwe juu yenu mnapoyaanza maisha mapya ya ndoa. Vijana
wakakomba mibaraka kibao toka madhabahuni! Ikawafurika mpaka myoni!
wakakomba mibaraka kibao toka madhabahuni! Ikawafurika mpaka myoni!
Punde tu Emma akapata ajira ya ulinzi........
anaangalia kushoto na kulia kama usalama upo maana ameshamiliki
so lazima ahakikishe usalama upo na amlinde!
anaangalia kushoto na kulia kama usalama upo maana ameshamiliki
so lazima ahakikishe usalama upo na amlinde!
Sauti ndogo inatoka.... Hivi Stella unajua nakupenda mke wangu? Nae anajibu
huju ameinamisha kichwa. Mmmmmh! najua sinimeona?
huju ameinamisha kichwa. Mmmmmh! najua sinimeona?
Subscribe to:
Posts (Atom)