MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, August 29, 2013

TAHARUKI YA BOMU K.K.K.T KIJITONYAMA MAJUZI

JUZI (Jumapili) Tarehe 25 Septemba 2013, hali ya taharuki ilizuka kwa waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam baada ya kuonekana kifaa cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kilichosadikiwa kuwa bomu.
Kifaa hicho ambacho kilifungwa katika boksi kilikutwa juu ya transfoma iliyoko nyima ya jengo la kitega uchumi cha kanisa hilo umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana, Mtabiri Mwandamizi wa TMA, Agustine Kanemba alisema kifaa hicho huwa kinarushwa kila siku kwenda angani kwa urefu wa kilometa 55,000 kikiwa kimeambatana na puto.
Alisema kikifika huko puto hupasuka na kusababisha kifaa hicho kudondoka chini jambo ambalo linasababisha wao kupata taarifa za hali ya hewa ya anga baada ya hatua hiyo. Lakini mara nyingi kifaa hicho hudondokea baharini.

 Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kijitonyama

 Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Hilo ambalo nyuma yake ndipo ilipo transformer kilipokuwa kifaa hicho kilichodhaniwa kuwa ni bomu.

 Hiki ndicho kifaa cha Mamlaka ya hali ya hewa TMA Kilichodhaniwa kuwa ni Bomu

 Mtaalamu akiangalia kifaa hicho

 Wataalamu hawa wakiondoa kamba iliyokuwa imefungwa kwenye kifaa hicho.

 Wataalam wakifanya bidii za kukitoa kifaa hicho kwenye transformer

 Tokea kushoto ni Michael Mwalwisi na Lukio Mjema wakikiangalia kifaa hicho kwa umakini

 Ni kama anasema....Jamani hili sio bomu ni kifaa cha kupimia hali ya hewa.

 Waumini na wananchi wakikiangalia kifaa hicho kwa karibu

 Waumini wakipata maelezo toka kwa mtaalamu kuhusiana na kifaa hicho.

 Watu wakifurahi baada ya kuhakikishiwa usalama wao

Watu wa Emergency wa kampuni ya umeme TANESCO walifika pia kuhakiki usalama.
 
Wakiondoka baada ya hali ya taharuki kutoweka

1 comment:

  1. Swali, kifaa cha kupima hali ya hewa kiliingiaje eneo la kanisa bila uongozi wa kanisa kuwa na taarifa?

    ReplyDelete