Neema Gaspal |
Neema Gaspel Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Anategemea kuwa
na Tamasha la Uzinduzi wa Album yake ya kwanza, Tamasha ambalo litafanyika
katika Ukumbi wa Ubungo Plaza siku ya Tarehe 1 Septemba 2013.
Album hiyo inayojulikana kwa jina la SHUJAA iliyobeba nyimbo
nane ambazo ni:
1.Shujaa
2.Mweleze Yesu
3.Machozi Yako
4.Nimekukimbilia Bwana
5.Ee Mungu
6.Kristo
7.Faida
8.Kwa Neema
Neema Gaspel Akizungumza na Christian Bloggers (Hawapo kwenye Picha) |
Lengo kuu la uzinduzi huo likiwa ni kusaidia watoto yatima
na wajane kwa asilimia Fulani ya kiasi kitakachopatikana siku hiyo, Huku
akisindikizwa na waimbaji Rose Mhando, Bahati Bukuku, Madam Ruth, Martha
Mwaipaja, Everine Msoma, Ambwene Mwasongwe, Mwanamapinduzi Maximilian Machumu,
Edson Mwasabwite, Enock Jonan a Wengine wengi.
Mgeni rasmi Atakuwa Mh. Samuel Sitta Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Atakayeongoza jopo la wageni mbalimbali kuzindua na
kumuunga mkono Neema.
Viingilio siku hiyo vitakuwa kama ifuatavyo.
Viti Maalum 10,000/=
Kawaida
Wakubwa 5,000/=
Watoto 2,000/=
Tiketi zinapatikana Praise Power Radio, Wapo Radio pia zitapatikana siku hiyo
mlangoni siku ya tamasha. Watu 50 wa kwanza watapata zawadi kama Lotion kutoka
kwa wadhamini wa tamasha hilo Grace Products. Pia Kutakuwa na Fashion Show
pamoja na mashindano ya ngumi na kudance. Usipange kukosa.
No comments:
Post a Comment