MESSAGE
MESSAGE
Pages
Thursday, August 29, 2013
ASKOFU MOSES KULOLA HATUNAYE TENA
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.
Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa watu wa ndani mwa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.
Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.
Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr. Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.
TAHARUKI YA BOMU K.K.K.T KIJITONYAMA MAJUZI
JUZI (Jumapili) Tarehe 25 Septemba 2013, hali ya taharuki ilizuka kwa waumini wa Kanisa la
KKKT Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam
baada ya kuonekana kifaa cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
kilichosadikiwa kuwa bomu.
Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kijitonyama
Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Hilo ambalo nyuma yake ndipo ilipo transformer kilipokuwa kifaa hicho kilichodhaniwa kuwa ni bomu.
Hiki ndicho kifaa cha Mamlaka ya hali ya hewa TMA Kilichodhaniwa kuwa ni Bomu
Mtaalamu akiangalia kifaa hicho
Wataalamu hawa wakiondoa kamba iliyokuwa imefungwa kwenye kifaa hicho.
Wataalam wakifanya bidii za kukitoa kifaa hicho kwenye transformer
Tokea kushoto ni Michael Mwalwisi na Lukio Mjema wakikiangalia kifaa hicho kwa umakini
Ni kama anasema....Jamani hili sio bomu ni kifaa cha kupimia hali ya hewa.
Waumini na wananchi wakikiangalia kifaa hicho kwa karibu
Waumini wakipata maelezo toka kwa mtaalamu kuhusiana na kifaa hicho.
Watu wakifurahi baada ya kuhakikishiwa usalama wao
Kifaa hicho ambacho kilifungwa katika boksi kilikutwa juu ya transfoma iliyoko nyima ya jengo la kitega uchumi cha kanisa hilo umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana, Mtabiri Mwandamizi
wa TMA, Agustine Kanemba alisema kifaa hicho huwa kinarushwa kila siku
kwenda angani kwa urefu wa kilometa 55,000 kikiwa kimeambatana na puto.
Alisema kikifika huko puto hupasuka na kusababisha kifaa hicho
kudondoka chini jambo ambalo linasababisha wao kupata taarifa za hali ya
hewa ya anga baada ya hatua hiyo. Lakini mara nyingi kifaa hicho hudondokea baharini.
Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Hilo ambalo nyuma yake ndipo ilipo transformer kilipokuwa kifaa hicho kilichodhaniwa kuwa ni bomu.
Hiki ndicho kifaa cha Mamlaka ya hali ya hewa TMA Kilichodhaniwa kuwa ni Bomu
Mtaalamu akiangalia kifaa hicho
Wataalamu hawa wakiondoa kamba iliyokuwa imefungwa kwenye kifaa hicho.
Wataalam wakifanya bidii za kukitoa kifaa hicho kwenye transformer
Tokea kushoto ni Michael Mwalwisi na Lukio Mjema wakikiangalia kifaa hicho kwa umakini
Ni kama anasema....Jamani hili sio bomu ni kifaa cha kupimia hali ya hewa.
Waumini na wananchi wakikiangalia kifaa hicho kwa karibu
Waumini wakipata maelezo toka kwa mtaalamu kuhusiana na kifaa hicho.
Watu wakifurahi baada ya kuhakikishiwa usalama wao
Watu wa Emergency wa kampuni ya umeme TANESCO walifika pia kuhakiki usalama.
Wakiondoka baada ya hali ya taharuki kutoweka
Wednesday, August 28, 2013
NEEMA GASPAL KUIBUKA NA ALBAMU YA SHUJAA
Neema Gaspal |
Neema Gaspel Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Anategemea kuwa
na Tamasha la Uzinduzi wa Album yake ya kwanza, Tamasha ambalo litafanyika
katika Ukumbi wa Ubungo Plaza siku ya Tarehe 1 Septemba 2013.
Album hiyo inayojulikana kwa jina la SHUJAA iliyobeba nyimbo
nane ambazo ni:
1.Shujaa
2.Mweleze Yesu
3.Machozi Yako
4.Nimekukimbilia Bwana
5.Ee Mungu
6.Kristo
7.Faida
8.Kwa Neema
Neema Gaspel Akizungumza na Christian Bloggers (Hawapo kwenye Picha) |
Lengo kuu la uzinduzi huo likiwa ni kusaidia watoto yatima
na wajane kwa asilimia Fulani ya kiasi kitakachopatikana siku hiyo, Huku
akisindikizwa na waimbaji Rose Mhando, Bahati Bukuku, Madam Ruth, Martha
Mwaipaja, Everine Msoma, Ambwene Mwasongwe, Mwanamapinduzi Maximilian Machumu,
Edson Mwasabwite, Enock Jonan a Wengine wengi.
Mgeni rasmi Atakuwa Mh. Samuel Sitta Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Atakayeongoza jopo la wageni mbalimbali kuzindua na
kumuunga mkono Neema.
Viingilio siku hiyo vitakuwa kama ifuatavyo.
Viti Maalum 10,000/=
Kawaida
Wakubwa 5,000/=
Watoto 2,000/=
Tiketi zinapatikana Praise Power Radio, Wapo Radio pia zitapatikana siku hiyo
mlangoni siku ya tamasha. Watu 50 wa kwanza watapata zawadi kama Lotion kutoka
kwa wadhamini wa tamasha hilo Grace Products. Pia Kutakuwa na Fashion Show
pamoja na mashindano ya ngumi na kudance. Usipange kukosa.
JOSEPHINE MINZA NKILA KUTOKA NA VIDEO YA MAISHA YA IBADA
Josephine Minza Nkila |
Akizungumza na waandishi wa habari Minza alisema video yake imesheheni jumla ya nyimbo 10 zenye maadhi ya slow (Worship Music), Kwaito na kadhalika.
Pia siku hiyo anategemea kupiga nyimbo zake katika mfumo wa LIVE Music.
Samuel Yona |
Abednego Hango, Ipyana Kibona, Prisca Kangi, David Yona, Jenifer Mushi na Samuel Yona ambaye ndiye producer aliyeisuka album hiyo.
Kama inavyoonekana katika picha hapo juu ni wakati video hiyo ikirekodiwa, Usikose siku hiyo.
Wednesday, August 7, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)