MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, December 30, 2013

CVC WAFANYA SILVER JUBILEE

AIC Chang'ombe Vijana Choir jana wamefanya sherehe kubwa ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya hiyo. Sherehe hizo zilifanyika kanisani kwao eneo la Chang'ombe Sokota. Katika ibada iliyosheheni kwaya nyingi ikiwemo kwaya ya AIC Shinyanga, AIC Dar es Salaam Choir, Neema Gospel Choir (AIC), Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Kwaya ya Unjilisti Mtoni (Lulu), Kwaya ya Ukombozi toka K.K.K.T Msasani. Katika kuadhimisha miaka 25 ya kwaya hiyo pia walizindua jina jipya la kwaya yao na kuwa AICT Chang'ombe Choir na CVC kubaki kuwa Brand Name. 

 Watumishi wa Mungu walikuwepo na kuhudumu katika ibada hiyo.


 Kwaya ya watoto ya AICT Chang'ombe

 Kwaya ya wenyeji AICT Chang'ombe Choir



 Rose Jefa mwimbaji toka Kenya

 Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama

 Kwaya ya AIC Shinyanga 

 Wana LULU toka Mtoni

 MC Tito ndiye aliyeongoza jahazi 

 Keki ya miaka 25


 Hawa ni vijana wa kanisani hapo wenye umri wa miaka 25 waliobahatika kula keki hiyo.

 Mwenyekiti wa AICT Chang'ombe Choir akikata keki

 Walezi wa kwaya tangu kuanzishwa kwake

 Baadhi ya watunzi wa nyimbo zilizobeba albamu tangu kuanzishwa kwa kwaya hiyo.

 Askofu Salala akizindua jina jipya la AICT Chang'ombe Choir

Kikundi cha wagaratia wakipozi katika picha na watumishi wa Mungu

Thursday, December 5, 2013

KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA KUFANYA SHEREHE ZA JUBILEE YA MIAKA 25


Jumapili hii ni hekaheka, Katika viwanja vya K.K.K.T Kijitonyama, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama watakuwa na sherehe za kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake. Kwaya hii iliyoanzishwa miaka 25 iliyopita imejulikana sana kwa nyimbo zake zikiwemo Hakuna Mungu Kama Wewe, Simba wa Yuda, Hakuna Mwanaume Kama Wewe, Ndani ya Safina, Tone la Damu na Album yao mpya iliyoko sokoni inayofahamika kwa jina la Namtangaza Kristo. Sherehe hizo zitafanyika katika ibada ya tatu inayoanza saa nne asubuhi kanisani hapo na kisha kufuatiwa na tamasha kubwa litakaloanza saa saba mchana litakaloshirikisha kwaya kongwe toka Arusha maarufu kwa Jina la Tumaini Shangilieni toka kanisa la St. James Anglican lililoko Arusha na pia kwaya zote za kanisa la K.K.K.T Kijitonyama.

 Na kama haitoshi Kwaya ya Uinjilisti wataimba wimbo mmoja wa kwaya ya Tumaini Shangilieni na vivyo hivyo kwaya ya Tumaini Shangilieni kuimba wimbo mmoja wa Kwaya ya Kijito. Nyimbo hizi ni zile zenye majina ya Hakuna Mungu Kama Wewe.
Katika kuadhimisha tukio hilo kwaya ya Uinjilisti Kijito wataimba nyimbo zao za zamani (Enzi za Mwalimu) zilizotungwa tangu kwaya inaanzishwa, Pia wataimba na waimbaji wote wa zamani waliowahi kuimbia kwaya hiyo. Akiwemo Eliwinjuka, Albert Mafwenga, Joyce Kitale, Lilian Joshua Mlelwa na wengine wengi.
 Pia siku hiyo wanakwaya watagawiwa vyeti na kutunukiwa nishani za utumishi mwema tangu wale wa zamani na walio wapya walioimbia kwaya hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa kwaya ya Uinjilisti Kijito alisisitiza watu wafike wajionee wenyewe wasisubiri kusimuliwa. Na kwamba watu waje wajionee matendo makubwa ya Mungu aliyowafanyia katika kipindi cha miaka 25. Mwenyekiti alidokeza kuwa Kwaya zote siku hizo zitaimba LIVE CD zitasikilizwa nyumbani.

Thursday, August 29, 2013

ASKOFU MOSES KULOLA HATUNAYE TENA


Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa watu wa ndani mwa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr. Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.

TAHARUKI YA BOMU K.K.K.T KIJITONYAMA MAJUZI

JUZI (Jumapili) Tarehe 25 Septemba 2013, hali ya taharuki ilizuka kwa waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam baada ya kuonekana kifaa cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kilichosadikiwa kuwa bomu.
Kifaa hicho ambacho kilifungwa katika boksi kilikutwa juu ya transfoma iliyoko nyima ya jengo la kitega uchumi cha kanisa hilo umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana, Mtabiri Mwandamizi wa TMA, Agustine Kanemba alisema kifaa hicho huwa kinarushwa kila siku kwenda angani kwa urefu wa kilometa 55,000 kikiwa kimeambatana na puto.
Alisema kikifika huko puto hupasuka na kusababisha kifaa hicho kudondoka chini jambo ambalo linasababisha wao kupata taarifa za hali ya hewa ya anga baada ya hatua hiyo. Lakini mara nyingi kifaa hicho hudondokea baharini.

 Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kijitonyama

 Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Hilo ambalo nyuma yake ndipo ilipo transformer kilipokuwa kifaa hicho kilichodhaniwa kuwa ni bomu.

 Hiki ndicho kifaa cha Mamlaka ya hali ya hewa TMA Kilichodhaniwa kuwa ni Bomu

 Mtaalamu akiangalia kifaa hicho

 Wataalamu hawa wakiondoa kamba iliyokuwa imefungwa kwenye kifaa hicho.

 Wataalam wakifanya bidii za kukitoa kifaa hicho kwenye transformer

 Tokea kushoto ni Michael Mwalwisi na Lukio Mjema wakikiangalia kifaa hicho kwa umakini

 Ni kama anasema....Jamani hili sio bomu ni kifaa cha kupimia hali ya hewa.

 Waumini na wananchi wakikiangalia kifaa hicho kwa karibu

 Waumini wakipata maelezo toka kwa mtaalamu kuhusiana na kifaa hicho.

 Watu wakifurahi baada ya kuhakikishiwa usalama wao

Watu wa Emergency wa kampuni ya umeme TANESCO walifika pia kuhakiki usalama.
 
Wakiondoka baada ya hali ya taharuki kutoweka

Wednesday, August 28, 2013

NEEMA GASPAL KUIBUKA NA ALBAMU YA SHUJAA

Neema Gaspal


Neema Gaspel Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Anategemea kuwa na Tamasha la Uzinduzi wa Album yake ya kwanza, Tamasha ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza siku ya Tarehe 1 Septemba 2013.

Album hiyo inayojulikana kwa jina la SHUJAA iliyobeba nyimbo nane ambazo ni:
1.Shujaa
2.Mweleze Yesu
3.Machozi Yako
4.Nimekukimbilia Bwana
5.Ee Mungu
6.Kristo
7.Faida
8.Kwa Neema

Neema Gaspel Akizungumza na Christian Bloggers (Hawapo kwenye Picha)
 Lengo kuu la uzinduzi huo likiwa ni kusaidia watoto yatima na wajane kwa asilimia Fulani ya kiasi kitakachopatikana siku hiyo, Huku akisindikizwa na waimbaji Rose Mhando, Bahati Bukuku, Madam Ruth, Martha Mwaipaja, Everine Msoma, Ambwene Mwasongwe, Mwanamapinduzi Maximilian Machumu, Edson Mwasabwite, Enock Jonan a Wengine wengi.
Mgeni rasmi Atakuwa Mh. Samuel Sitta Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Atakayeongoza jopo la wageni mbalimbali kuzindua na kumuunga mkono Neema.
Viingilio siku hiyo vitakuwa kama ifuatavyo.
Viti Maalum 10,000/=
Kawaida
Wakubwa 5,000/=
Watoto 2,000/=
Tiketi zinapatikana Praise Power Radio, Wapo Radio pia zitapatikana siku hiyo mlangoni siku ya tamasha. Watu 50 wa kwanza watapata zawadi kama Lotion kutoka kwa wadhamini wa tamasha hilo Grace Products. Pia Kutakuwa na Fashion Show pamoja na mashindano ya ngumi na kudance. Usipange kukosa.

JOSEPHINE MINZA NKILA KUTOKA NA VIDEO YA MAISHA YA IBADA


Josephine Minza Nkila
Mwanadada Josephine Minza Nkila ambaye mara nyingi uhudumu na Mwalimu Mgisa Mtebe wa huduma ya Robbon Ministries. Anategemea kuachilia Video yake mpya itakayokuja kwa jina la MAISHA YA IBADA (LIFE OF WORSHIP) tarehe 22 September 2013. Video hiyo ambayo imechukuliwa live katika Ukumbi wa Upanga City Christian Centre, mahali ambapo Video hiyo itazinduliwa hapo hapo pia. 

Akizungumza na waandishi wa habari Minza alisema video yake imesheheni jumla ya nyimbo 10 zenye maadhi ya slow (Worship Music), Kwaito na kadhalika.
Pia siku hiyo anategemea kupiga nyimbo zake katika mfumo wa LIVE Music.


Samuel Yona
 Akishirikiana na wanamuziki wafuatao:
Abednego Hango, Ipyana Kibona, Prisca Kangi, David Yona, Jenifer Mushi na Samuel Yona ambaye ndiye producer aliyeisuka album hiyo.

 Kama inavyoonekana katika picha hapo juu ni wakati video hiyo ikirekodiwa, Usikose siku hiyo.

 

Wednesday, August 7, 2013

Tuesday, July 9, 2013

Katika Ibada K.K.K.T Kijitonyama Wiki Hii

Katika ibada wiki hii, Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kijitonyama uwepo wa Bwana ukiwa umeshuka. Pale waimbaji walipomtukuza Mungu kwa nyimbo na mapambio. Yaliyoimbwa na kwaya mbalimbali zilizosali ibada hiyo ya tatu, Ikiwemo kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Kwaya ya UKWATA Dar Pwani - Kikundi cha mkoa. Pia ibada hiyo ikiongozwa na watumishi wengine akiwemo Mwinjilisti Kipingu aliyeongoza ibada akishirikiana na Parish worker wa Usharika wakati Mwinjilisti Roserine Kambeyi aliyehubiri habari za Kufunguliwa. Pia mtumishi huyu anaendesha semina ya neno la Mungu wiki nzima katika usharika wa Kijitonyama. Akiwafanyia watu maombi ya kufungulia toka nguvu za giza. Wenye mapepo na wagonjwa mbalimbali wakifunguliwa kwa jina la Yesu.

Habari katika picha:
 Mwinjilisti Leonard Kipingu akishirikiana na Parish Worker wakiongoza ibada

Kwaya ya UKWATA Dar Pwani - Kikundi cha mkoa wakimwimbia Mungu katika ibada. Vijana hawa ambao wamefanikiwa kutoa albamu yao "KAMA INAVYOONEKANA KWENYE PICHA HAPO CHINI" walikuwa wakiiuza cku hiyo baada ya ibada. Jipatie nakala yako umtukuze Mungu pamoja nao. Wasiliana nao kwa namba za simu zilizo hapo chini kwenye picha.

 Mwonekano wa CD ya Kwaya ya UKWATA Dar Pwani - Kikundi cha mkoa

 Na huu ndio mwonekano wa cover la albamu ya Kwaya ya UKWATA Dar Pwani - Kikundi cha mkoa

 Praise Team wakiliongoza Kanisa katika ibada ya kuabudu.

 Wanamuziki waliotumika katika ibada hiyo wakivipiga vyombo vyao katika hali ya kuabudu

 Upako unapowashukia wana muziki mambo huwa hivi, huku mafundi mitambo wakiwa busy kuweka mitambo sawa.

 Pichani anaonekana mama Anastazia Mujumba (Mwenye browse nyeusi) akimsikiliza Mwinjilisti alihudhuria yeye na jamaa yake pamoja na marafiki kumtukuza na kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 80. Pamoja na shukurani hiyo mama huyo alimtolea Mungu shukrani kwa kazi za mikono yake. Pamoja na uzee huo lakini bado anweza kufanya kazi za mikono. Kulia ni mwanae Proscovia Mujumba.

 Mwinjilisti Kipingu akiomba baraka kwa Mama Anasatazia Mujumba

 Katika mahubiri huyu ndiye Mwinjilisti Roserine Kambeyi akijaa upako na nguvu za roho mtakatifu akihubiri habari za watu kufunguliwa toka vifungo vya mwovu shetani. Usikose kuhudhuria semina wiki hii.

 Mwinjilisti Kipingu akisoma Ujumbe wa mama Anastazia katika sadaka aliyoitoa uliosemeka... Hataka katika hali ya uzee huu, namshukuru Mungu anayeniwezesha kufanya kazi kwa mikono yangu"

 Hizi ni moja ya kazi anazozifanya mama Anasatazia, wakati zikinadishwa. Aliyeshi nguo tokea kushoto ni Everlight Matinga na bi Proscovia Mujumba

 Ikiwa imepita wiki moja baada ya harambee ya Kuchangia Mfuko wa Elimu katika Usharika wa kijitonyama. Watu walionekama kuendelea kuchangia mfuko huo kwa kuchukua kadi za bei mbalimbali zinazopatikana usharikani Kijitonyama. Huku wengine wakirudisha kadi hizo na pesa na kupewa risiti zao.
 
 Mhasibu wa Usharika Bw. Nicodemus Lekei aliyekuwa akitoa kadi hizo na kupokea fedha zilizochagishwa.

 Mwinjilisti Kipungu akisema neno la shukurani kuhairisha ibada hiyo