MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, February 7, 2011

Edmund Hatunaye Tena

Wapendwa Jana Mchana Tumepokea Taarifa za Kusikitisha. Baada ya Ibada Mchungaji Alitangaza Kwamba Tumeondokewa na Mpendwa Wetu Edmund Mushi. Wengi Wetu Tunamfahamu Kama Mzee wa Kanisa pia Mwenyekiti wa Kwaya ya Uinjilisti.Hivyo Msiba Upo kwake Kimara Suka. Na Mwili wa Marehemu Utasafirishwa Kesho JumanneKuelekea Moshi kwa Mazishi.Tulimpenda Sana Lakini Mungu kampenda Zaidi.Bwana Ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana Libarikiwe.

5 comments:

  1. Poleni wanafamilia ya Kijitonyama.Hiyo ndio njia yetu kila mmoja, hivyo analotukumbusha ni kujiweka tayari maana hatuijui siku wala saa.

    ReplyDelete
  2. Mungu ampe pumziko la milele na amani kwa kweli kaka yetu aliumwa sana na tulitaka aamke ili kufanya kazi ya Mungu lakini Mungu akasema amesha maliza zamu yake, nasi hatuna budi kumtukuza Mungu maana yeye ndiye aliyetupa Edmund na yeye ndiye aliyemtwaa, jina lake na libarikiwe

    ReplyDelete
  3. Poleni sana Kijito. Mungu afanyike faraja kwa familia, kwaya, usharika na kanisa kwa ujumla. Mungu awatangulie mnapojiandaa kuupumzisha mwili wake kwenye nyumba ya milele.
    Sisi tulio hai bado tuna kazi kubwa ya kumfanyia Mungu, hebu tusimame katika zamu zetu.

    ReplyDelete
  4. Kweli Edmund amemaliza kazi yake aliyotumwa duniani. Mungu mwenyewe agange mioyo yetu na kutupa faraja. Ni kazi yetu kusimama katika zamu zetu na kuifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu, kwani hatujui siku wala saa. Mungu wetu atukuzwe daima katika maisha yetu.

    ReplyDelete
  5. Poleni sana wapendwa wetu wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, na zaidi kwa familia ya marehemu. Bwana amemwita ndugu yetu Edmund naye ameitika, kama alivyoitika katika uhai wake kumuitikia katika kufanya kazi zake, basi tuzidi kumuomba mungu ampuzishe kwa amani. Kwa wana familia na kwaya ya kijitonyama tunamuomba mwenyeze mungu awajalie moyo wa uvumilivu na upole katika maombolezo haya.

    ReplyDelete