MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Upendo Nkone ni
miongoni mwa wasanii wa ndani watakaopamba Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Upendo anakuwa msanii wa tatu wa ndani kutangazwa atashiriki
katika tamasha hilo baada ya Rose Muhando na John Lissu ambao walitangazwa
Ijumaa na Jumamosi.
Akizungumza Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema mwaka huu katika tamasha hilo
wanawapa mashabiki kile wanachokitaka."Tunaendesha maoni kwa mashabiki wetu wapendekeze wasanii
gani wawepo, hivyo hao watatu ndiyo mpaka sasa wameshika nafasi za juu kwa
kupendekezwa sana na mashabiki.
Wengine tutawatangaza kadri mambo yatakavyokuwa mazuri na
pia tukiwa tumezungumza nao juu ya ushiriki wao,"alisema Msama.
Tamasha la Pasaka
litafanyika Dar es Salaam Machi 31, kisha siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya,
Aprili 3 itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri Dodoma
na Aprili 7 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo
ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo
Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava,
Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.Pia kwaya
mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku
hiyo.
Picha ya wasanii na choir zilizohudumu Tamasha la pasaka mwaka 2012
Habari kwa hisani ya blog ya michuzi, www.issamichuzi.blogspot.com
Habari kwa hisani ya blog ya michuzi, www.issamichuzi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment