MESSAGE
MESSAGE
Pages
Thursday, March 7, 2013
Askofu Bandia afanikiwa Kupenyeza na Kuingia Kwenye Mkutano wa Makadinali
Mtu aliyejifanya Kardinali wa Kanisa Katoliki, Ralph Napierski (kushoto) akisalimiana na Kardinali Sergio Sebiastiana. Napierski alikamatwa akijaribu kuingia kwenye mkutano wa makardinali unaoendelea Vatican
Vatican, Italia
Askofu bandia amefanikiwa kujipenyeza na kuingia kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya.
Askofu huyo bandia, Ralph Napierski ambaye ni mzawa wa Ujerumani alifanikiwa kujipenyeza na kusalimiana kisha kupiga picha za kumbukumbu na baadhi ya makadinali waliopo kwenye mkutano huo bila kugundulika.
Uzamiaji wake ambao ulileta mashaka kuhusu uimara wa usalama eneo hilo wanapokutana makadinali 103, ambao wamekusajika kwenye Makao Makuu ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya, huku wengine 12 wakiwa hawajawasili.
Katika mkutano huo, Kadinali wa juu kutoka Uingereza, Cormac Murphy O'Connor pia anahudhuria.
Napierski alionekana akisalimiana na Kadinali Sergio Sebiastiana nje ya ukumbi wa Papa Paul VI akiwa hajatambua kuwa siyo miongoni mwa wenzake, huku akiwa amezungukwa na makasisi wengine wa kanisa hilo ambao pia hawakuweza kutambua.
Walinzi wa kundi la Swiss Guars linaloshughulika na ulinzi wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican, walimbaini kuwa siyo miongoni mwa wahusika kutokana na vazi lake alilofunga kiunoni, ambalo siyo sahihi bali ulikuwa ni mtandio uliokunjwa vizuri.
Pamoja na vazi hilo la rangi ya zambarau kutokuwa sahihi, pia kofia aliyokuwa ameivaa haikuwa miongoni mwa zile zinazotambulika kuvaliwa na viongozi wa kanisa hilo.
Tofauti nyingine iliyobainika ni ufupi wa kanzu yake na rozari aliyovaa haikuwa halisi, kwa kuwa ilikuwa ni fupi kuliko wanazotumia viongozi wa kanisa hilo.
Kabla ya kubainika, Napierski alijitambulisha kwa waandishi wa habari kwamba jina lake ni Basilius ni miongoni mwa wawakilishi wa Kanisa la Orthodox kutoka Italia.
Awali, kulikuwa na taarifa kwamba aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Kanisa Katoliki limefanya “Kosa kubwa” kwa kuwaruhusu makasisi wanaotuhumiwa kwa makosa ya ngono kubadilishwa kutoka maeneo yao ya awali na kupelekwa kwingine, kuficha kashfa zao badala ya kuzishughulikia.
Mtuhumiwa huyo ambaye baada ya kubainika aliondolewa eneo hilo, anaongoza tovuti ambayo aliitumia kujitambulisha kwamba yeye ni kasisi kupitia Shirika la Kikatoliki la Corpus Dei, huku akiwa amevaa mavazi ya kikasisi na kujidhihirisha kama “Mtumwa na Nabii kama Mtakatifu Paul”.
Msemaji wa Kanisa Katoliki mjini Vatican, Federico Lombardi alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa yoyote na muda wote alikuwa akishughulika katika mkutano.
Source: Mwananchi.
Monday, March 4, 2013
UPENDO NKONE ANG'ARA TAMASHA LA PASAKA
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Upendo Nkone ni
miongoni mwa wasanii wa ndani watakaopamba Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Upendo anakuwa msanii wa tatu wa ndani kutangazwa atashiriki
katika tamasha hilo baada ya Rose Muhando na John Lissu ambao walitangazwa
Ijumaa na Jumamosi.
Akizungumza Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema mwaka huu katika tamasha hilo
wanawapa mashabiki kile wanachokitaka."Tunaendesha maoni kwa mashabiki wetu wapendekeze wasanii
gani wawepo, hivyo hao watatu ndiyo mpaka sasa wameshika nafasi za juu kwa
kupendekezwa sana na mashabiki.
Wengine tutawatangaza kadri mambo yatakavyokuwa mazuri na
pia tukiwa tumezungumza nao juu ya ushiriki wao,"alisema Msama.
Tamasha la Pasaka
litafanyika Dar es Salaam Machi 31, kisha siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya,
Aprili 3 itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri Dodoma
na Aprili 7 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo
ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo
Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava,
Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.Pia kwaya
mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku
hiyo.
Picha ya wasanii na choir zilizohudumu Tamasha la pasaka mwaka 2012
Habari kwa hisani ya blog ya michuzi, www.issamichuzi.blogspot.com
Habari kwa hisani ya blog ya michuzi, www.issamichuzi.blogspot.com
Sunday, March 3, 2013
AFLEWO TANZANIA 2013 BISHOP BREAKFAST YAFANA
Katika Kuelekea Event ya Aflewo Tanzania 2013,Siku ya jana ilikuwa
Bishops Breakfast Forum katika Hotel ya Regency Park Mikocheni,ikiwa ni
katika kuwashirikisha Maaskofu na Mtume wa huduma mbalimbali maono na
maana ya kuwepo kwa Aflewo Tanzania mwaka 2013.
Mnamo terehe 5-5-2013 BCIC Mbezi Beach itakuwa ni usiku wa aina yake katika Kumsifu na Kumwabudu Mungu ambapo Aflewo Mass Choir yenye waimbaji zaidi ya 90 watapaza sauti zao wakiimba sifa kwa Mungu.
Katika Bishops Breakfast hiyo iliyoudhuliwa na baadhi ya Maaskofu kama
Apostle Ntepa,Bishop Fredie Kyara, Bishop Elly Mwende,Bishop Simtovu,Bishop Mwasota, Bishop Shegga, Pastor Fredie (UpperRoom Minisry )Bishop Gamanywa alitoa hudhuru kwa Kuwalilishwa na Pastor Amoni Kalahilo na wengine wengi na kusifu Aflewo kuweza kuwa kutanisha na wao kama Maaskofu katika Jiji la Dar es salaam kuwashirikisha Maono ya Aflweo Tanzania na kusifu juhudi zinafanywa maana ni katika Kuujenga mwili wa Kristo na kulileta pamoja Kanisa la Tanzania na Afrika Kwa Ujumla.
Pastor Paul Safari na Abel Orgenes Kama walezi wa huduma ya Aflewo Tanzania,wakieleza umuhimu wa huduma hiyo kwa waimbaji ni pamoja na kukua kwa maisha ya kiroho kati ya waimbaji na Mungu maana tofauti na uimbaji pia kuna mafundisho kuhusu Maisha ya wokovu na Maana ya Kufisu na Kuabudu kwa ujumla
Pastor Fredie Kyara aliweza kutoa ushuhuda wa jinsi Mkesha huo ulivyo wa baraka sana kwa kusema jinsi ilivyoweza kukutana na uwepo wa Mungu kwa Mkesha uliopita mwaka 2012,na kusihi Maaskofu wengine kukubali na kuunga mkono huduma hii ya Aflewo kwa kuwa ruhusu waumini wao makanisani kuhusika kikamilifu.
Kwa kumalizia Maaskofu hao walipata nafasi ya kuchangia na kusema kuwa wanakubaliana kwa nia moja na kusema wako tayari kushiriki kwa namna moja au nyingine kuhakikisha mkesha wa Aflewo Tanzania 2013 unafanikiwa."
Subscribe to:
Posts (Atom)