MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, July 15, 2012

KIJITO JUMAPILI HII

Kwa mara nyingine tena katika hema ya kukutania ya Kijito, Bwana Yesu alitamalaki katika ibada ambayo iliongozwa na Mchungaji Ernest Kadiva ambaye ndiye mchungaji kiongozi aliyehubiri upendo akisisitiza wakristo kupendana na kuchukuliana. Ibada ambayo iliambatana na Praise and Worship toka kwa Praise Team ya kanisani hapo. Angalia matukio katika picha
 Praise Team ikiongozwa na kiongozi wa sifa Allen, 
wakimsifu Mungu wakati wa kipindi cha kusifu na kuabudu

 Sehemu ya kanisa wakimsifu Mungu 

Upande mwingie wa kanisa wakimsifu Mungu, hili limekuwa suala la kawaida kwa washarika wa Kijitonyama kucheza mbele za Bwana, hata wazee.  
Sehemu ya kwaya kuu wakiimba na kucheza wakati wa sifa

 Wakristo walimtolea Mungu sadaka ya shukrani 
wakati wa ibada wakipokea baraka toka kwa Mchungaji
 Kwaya ya Uamsho wakiwa tayari kumsifu Mungu katika ibada

 Mtumishi wa Mungu na mwana Praise Team,
 Heri Nyambo akimshukuru Mungu mbele ya kanisa baada 
ya Mungu kusikia maombi yake kumpatia mwenzi

Mchungaji Ernest Kadiva akiwa madhabahuni akihubiri
Hatimaye ibada ikafungwa kwa maombi

Wapendwa kuweni makini na mtu huyu, Amekamatwa leo akikwapua mkoba wa mtu wakati mwenye mkoba amekwenda mbele kutoa sadaka. Ndipo bwana huyu akapata nafasi ya kuupitia kwenye bench alipokuwa ameuacha na baadae kukamatwa na walinzi wa kanisa kabla hajatoweka.

No comments:

Post a Comment