MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, July 26, 2012

YALIYOJIRI IMUKA SINGERS CONCERT

Jumapili ya tarehe 22 Julai, Gospel House of Talent Tanzania pamoja na COSAD Tanzania walijumuika pamoja kuwaleta Tamashani Imuka Singers. Imuka Singers ambao ni kwaya toka mkoa wa Kagera waliounda kundi hilo toka katika kwaya mbalimbali toka mkoani humo.  Waliandaa tamasha hilo wakiwa na malengo ya kukusanya Milioni 150 za kitanzania ili ziwawezeshe katika kupata nauli ya kwendea nchini Marekani wanakotarajia kwenda muda mfupi ujao wakiwa na malengo ya kutangaza kazi ya Mungu, kutangaza taifa letu la Tanzania ikiwa ni pamoja na kuonesha kazi mbalimbali za sanaa wanazofanya kwa mikono yao.

Hivi ndivyo yalivyokuwa matukio mbalimbali katika tamasha hilo

 Gospel House Of Talent ndio waliotuandalia haya


 Mwanadada akiimba muziki wa injili on the stage ndie aliye fungua dimba

 Akiwa na dancers wake wakilitawala jukwaa


 Mwimbaji mwingine wa nyimbo za injili, mtanzania aishiye Zambia nae akahubiri kwa njia ya nyimbo

 Kwaya ya Uinjilisti Kijito nao walikuwepo, hapa wakiimba nyimbo za kuabudu kukaribisha uwepo wa Mungu kabla ya ufunguzi rasmi wa tamasha hilo

 Wakiwa kiroho zaidi

 Hudson Kamoga a.k.a HK2 Akiwa kiroho zaidi

 Hudson Kamoga ambaye ndiye alikuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo, akiabudi na kwaya ya uinjilisti Kijito

 Askofu Benson Bagonza wa K.K.K.T Dayosisi ya Karagwe akiwa na mwenyeji wake Smart Baitani ambaye ndiye organiser wa tamasha hilo

 Askofu Bagonza akifungua tamasha kwa maombi

 The Voice wakimtukuza Mungu kwa nyimbo za injli kwa style yao ya Acapela 

 wakiwa kiroho zaidi

 Jane Miso mamaa wa Omoyo akiimba

 Akiwa amelitawala jukwaa huku kila mtu akiimba omoyo

 Meza ya wageni rasmi wakiwa wakiwa wamesimama wakicheza mbele za Bwana baada ya sifa kutawala

 Hatimaye Upendo Nkone na Upendo wa Yesu wanizunguka

 Huku na huku na pale, kama mawimbi...

 Siku hiyo aliimba live akisindikizwa na kwaya ya Uinjlisiti Kijito

 Mwanadada Christina Shusho uvumilivu ukawa 0 akaja kumtunza rafiki yake

 Hapa Shusho akiyarudi na Upendo Nkone

 HK2 Akiwahabarisha watu nini kinajiri

 Smart Baitani akiwakaribisha Imuka Singers on the stage

 Haooooo Imuka Singers wakiwa kitamaduni zaidi

 Aaaah wanacheza hao, duh

 Mitaa ya mangoma ndo hii hapa!

 Kwa style mbalimbali za utamaduni wa mkoa wa Kagera kila mtu yuko fit katika kucheza

 HK 1 Haris Kapiga akinena jambo

 Upendo Nkone, Jane Misso na Martha Mwaipaja wakisifu na kucheza

 Hudson Kamoga akicheza baada ya kuvutiwa na wimbo wa Christina Shusho

 Imuka baada kuimba nyimbo za Taifa la Tanzania, wakatoa shukrani zao

 Mkuu wa mkoa wa Kagera Canal Fabia Massawe akiweka msisitizo wa watu kuwachangia Imuka Singers katika kutekela azma yao

 Martha Mwaipaja hakukosa katika stage na nyimbo zake huku akitabasam

 Jane Misso akapanda jukwaani kumuunga mkono Martha Mwaipaja

 Hapa uvumilivu ukawa 0 kwa waimbaji wengine wakajikuta kwenye stage kumsindikiza Martha Mwaipaja

 Hatimaye Joshua Mlelwa na wimbo wake ni wewe utendaye maajabu akaimba live na kwaya ya uinjilist Kijito

 Jamaa akiwa stejini utampenda

 Hatimaye tamasha likaisha, wageni rasmi wakiagana

Friday, July 20, 2012

CONCERT CONCERT CONCERT

Don't Miss....This SUNDAY at Diamond Jubilee Jubilee, VIP All. Doors Open from 10AM Top Talent of Gospel Music From Tanzania including Jane Misso, Christina Shusho, Upendo Nkone, Bahati Bukuku, and More will join Imuka Singers for an unforgottable evening in Tanzania....For More details and Tickets call: +255.712.703.986 | +255.786.024.210 | www.imukasingers.org

Sunday, July 15, 2012

KIJITO JUMAPILI HII

Kwa mara nyingine tena katika hema ya kukutania ya Kijito, Bwana Yesu alitamalaki katika ibada ambayo iliongozwa na Mchungaji Ernest Kadiva ambaye ndiye mchungaji kiongozi aliyehubiri upendo akisisitiza wakristo kupendana na kuchukuliana. Ibada ambayo iliambatana na Praise and Worship toka kwa Praise Team ya kanisani hapo. Angalia matukio katika picha
 Praise Team ikiongozwa na kiongozi wa sifa Allen, 
wakimsifu Mungu wakati wa kipindi cha kusifu na kuabudu

 Sehemu ya kanisa wakimsifu Mungu 

Upande mwingie wa kanisa wakimsifu Mungu, hili limekuwa suala la kawaida kwa washarika wa Kijitonyama kucheza mbele za Bwana, hata wazee.  
Sehemu ya kwaya kuu wakiimba na kucheza wakati wa sifa

 Wakristo walimtolea Mungu sadaka ya shukrani 
wakati wa ibada wakipokea baraka toka kwa Mchungaji
 Kwaya ya Uamsho wakiwa tayari kumsifu Mungu katika ibada

 Mtumishi wa Mungu na mwana Praise Team,
 Heri Nyambo akimshukuru Mungu mbele ya kanisa baada 
ya Mungu kusikia maombi yake kumpatia mwenzi

Mchungaji Ernest Kadiva akiwa madhabahuni akihubiri
Hatimaye ibada ikafungwa kwa maombi

Wapendwa kuweni makini na mtu huyu, Amekamatwa leo akikwapua mkoba wa mtu wakati mwenye mkoba amekwenda mbele kutoa sadaka. Ndipo bwana huyu akapata nafasi ya kuupitia kwenye bench alipokuwa ameuacha na baadae kukamatwa na walinzi wa kanisa kabla hajatoweka.