Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Jana imezindua Jengo la ghorofa tisa lijulikanalo kwa jina la Kijitonyama Lutheran Centre sambamba na uzinduzi mwingine wa nyumba ya ghorofa moja ambayo usharika wa Kijitonya umeinunua nayo ikiitwa Kijitonyama Lutheran Centre Annex. Uzinduzi huo ulifanywa na Askofu mkuu wa Kanisa hilo Dr.Alex Gehaz Malasusa. Gharama za ujenzi wa jengo hilo kubwa na ununuzi wa nyumba hiyo umeligharimu kanisa hilo takribani shilingi za kitanzania bilioni 3.5 Jengo hilo litatumika kwa shughuli za kiofisi na nyingine kama zitakavyobainishwa na hapo baadae.
Katika uzinduzi huo ulioambatana na ibada askofu huyo aliwaasa wakristo kujitokeza kwa wingi katika kuchangia mchakato wa kupata katiba mpya.
Katika uzinduzi huo ulioambatana na ibada askofu huyo aliwaasa wakristo kujitokeza kwa wingi katika kuchangia mchakato wa kupata katiba mpya.
Fuatana nami kwa tukio hilo katika picha.
Hilo ndilo jengo lililozinduliwa,Wanaoonekana kwenye picha ni wadau mbalimbali waliojihusisha katika kazi mbalimbali za kuhakikisha ujenzi hata uzinduzi unakwenda kama ulivyopangwa
Huu ni upande wa kushoto wa jengo hilo
Upande wa nyuma linaonekana hivi
Maandamano yalioongozwa na kundi la wapiga tarumbeta, kuelekea kwenye jengo hilo kwa shughuli ya uzinduzi
Watoto wa sunday school wa kanisa hilo nao wakiwa kwenye maandamano
Wazee wa kanisa wakiwa na nyuso za furaha na wakiwa katika hali ya utanashati na kupendeza nao walihusika katika maandamano hayo.
Parish wokers na watumishi wengine wa kanisa nao hawakuwa nyuma katika maandamano
Wachungaji wa sharika mbalimbali nao wakiwa kwenye maandamano
Na mwisho wa maandamano walikaa wakuu wa jimbo makatibu wa kuu pamoja na Askofu A.G. Malasusa
Viongozi,waumini na vikundi vya kwaya wakiwa tayari wakisubiri uzinduzi wa jengo hilo
Askofu Alex G. Malasusa akianza ibada ya uzinduzi wa jengo hilo
Jopo la watumishi wa Mungu wakisikiliza kwa makini
Kwa mbali ni kwaya aalikwa ya Winner toka Ubungo
Wazee wa kanisa nao wakiwa makini
Parish wokers nao pia wakiwa katika hali ya uchaji
Katibu wa baraza la wazee wa kanisa la Kijitonyama akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo
Eng. Sanyiel Kishimbo aliyekuwa msimamizi wa ujenzi huo nae akitoa taarifa kabla ya kulikabidhi kwa katibu wa dayosisi
Wakati ukafika na utepe ukakatwa tayari jengo likazinduliwa kelele za shangwe na vigelegele vikasikika
Askofu akiwa amegusa lango kuu la jengo hilo huku akibariki kila aingiaye na kutoka katika mjengo huo
Hii ni sehemu ya basement iliyomo ndani ya jengo hilo itakayotumika maalum kufundishia darasa la Sunday school kwa watoto wa kanisa hilo la Kijitonyama
Watoto wakaonyesha furaha yao kwa kuimba wimbo wakifurahia sehemu ya ukumbi huo itakayotumika kama darasa kwao
Hatua iliyofata ni ile ya kufungua sehemu ya jiwe la uzinduzi
Askofu Malasusa akifungua sehemu ya jiwe la ufunguzi
Jiwe la uzinduzi linaonekana hivi
Hii ndiyo Kijitonyama Lutheran Centre Annex kabla ya kuzinduliwa
Askofu Malasusa akizindua nyumba hiyo ya ghorofa moja kwa kukata utepe
Watumishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wazee wa kanisa wakipozi katika picha ya pamoja
Wachungaji wote waliokuwepo nao wakapozi katika picha ya pamoja
Kwaya ya Winners toka Ubungo wakihudumu katika ibada
Kwaya ya Umoja ya usharikani hapo wakihudumu katika ibada
Askofu Malasusa akihubiri
Hii ni kwaya ya uamsho, wakimwimbia Mungu wakati wa ibada