mwenzetu katika shamba la Bwana Dada Happiness Andrew.
Ambaye tumehudumu naye katika Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.
Kwa habari tulizopata ni kwamba marehemu alikuwa akiumwa.
Mauti imemkuta Mwanza akiwa kwa mdogo wake.
Tutaendelea kuwajuza tukipata habari zaidi
Rest In Peace Happiness
Zifuatazo ni picha za marehemu wakati wa uhai wake
Marehem wakati wa uhai wake katika huduma na wanakwaya wenzake.
Hapa ilikuwa Tamasha la UimbajiMarehemu na wanakwaya wenzake wakati wa shooting ya video ya kwaya ya uinjilisti ijulikanayo kama Ndani ya safina
Hii ilikuwa jumapili fulani hivi baada ya ibada, akaomba tupige picha nae.
Hapa tulikuwa naye katika huduma ya kutembelea watoto yatima wa kituo cha Kurasini ambayo kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama huwatembelea watoto hao kila mwaka
Akiwa na akina dada wenzake katika huduma siku hiyo waliita maalum kama kitenge day maana wengi wao walivaa nguo za vitenge. Hapa walikuwa usharika wa Makongo
Poleni sana kwa msiba huo. Mungu awe faraja yenu.
ReplyDeletePoleni sana na Mungu awape uvumilivu kwa wakati huu mgumu.
ReplyDelete