MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, August 29, 2011

Ni Pazuri

Wimbo mpya wa Kwaya ya Uinjilist Kijitonyama. Kwa mara ya kwanza uliimbwa terehe 24 Julai 2011 Katika ibada iliyofanyika usharikani kwao na baadae wakauimba kwenye tamasha la UKUD lilofanyika baadae usharika wa Msasani siku hiyo.









Friday, August 12, 2011

HAPPINESS ANDREW HATUNAYE TENA

Ni jana mida ya jioni tumepata taarifa ya kuondokewa na mtumishi
mwenzetu katika shamba la Bwana
Dada Happiness Andrew.
Ambaye tumehudumu naye katika Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.

Kwa habari tulizopata ni kwamba marehemu alikuwa akiumwa.
Mauti imemkuta Mwanza akiwa kwa mdogo wake.
Tutaendelea kuwajuza tukipata habari zaidi
Rest In Peace Happiness
Zifuatazo ni picha za marehemu wakati wa uhai wake




 Marehem wakati wa uhai wake katika huduma na wanakwaya wenzake. 
Hapa ilikuwa Tamasha la Uimbaji

 Marehemu na wanakwaya wenzake wakati wa shooting ya video ya kwaya ya uinjilisti ijulikanayo kama Ndani ya safina

 Hii ilikuwa jumapili fulani hivi baada ya ibada, akaomba tupige picha nae.

Hapa tulikuwa naye katika huduma ya kutembelea watoto yatima wa kituo cha Kurasini ambayo kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama huwatembelea watoto hao kila mwaka
Akiwa na akina dada wenzake katika huduma siku hiyo waliita maalum kama kitenge day maana wengi wao walivaa nguo za vitenge. Hapa walikuwa usharika wa Makongo