MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, January 11, 2016

K.K.K.T KIJITONYAMA WAFANYA IBADA YA KUPANDA MBEGU YA MWAKA 2016

Jana tarehe 10-01-2016 K.K.K.T Kijitonyama walifanya ibada maalum iliyojaa matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na shukrani kwa watu mbalimbali waliofika hapo kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea, mmoja wapo akiwa ni mama Julieth Mwakikoti aliyemshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 53 ya kuzaliwa. Pamoja na hayo watu walifika na sadaka mbali mbali ikiwa ni pamoja na ile ya fungu la kumi na sadaka ya kupanda mbegu ya kumkabidhi Mungu maisha na mipango yote waliyonayo kwa mwaka mzima. Ibada hiyo iliongozwa na Mwinjilisti Monyo. Huku Mhubiri akiwa John Sembatwa aliyegusa mioyo ya watu kwa neno la kupanda mbegu huku akimalizia kwa maombi kwa watu walioshindwa kusamehe na kuachilia watu waliowatendea mabaya. Pia aliombea watoto ili wakue kwa katika kicho wakimpendeza Mungu na wanadamu. Ibada ilimalizika kwa uzinduzi na kuwekwa wakfu kwa photocopier machine na computer 1 (laptop).

Yafuatayo ni matukio katika picha.
 Mwinjilisti Monyo akifanya maombi ya shukrani kwa familia ya mama Julieth Mwakikoko (mwenye nguo ya kijani aliyepiga magoti). Akimshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 53.

 Praise Team ya K.K.K.T Kijitonyama wakimtukuza Mungu wakati wa ibada

 Moja ya wana Praise Team akiongoza washarika kuimba Tenzi za Rohoni.

 Waumini wakimwabudu Mungu wakati ibada ikiendelea.

Praise Team wakimwandaa mtumishi wa Mungu Mwinjilisti John Sembatwa kabla ya mahubiri.

Mwinjilisti John Sembatwa akitafakari kabla ya kuanza mahubiri.


 Wakati akitoa neno la Mungu, Mwinjilisti John Sembatwa.

 Baada ya mahubiri watu wakiutafuta uso wa Bwana kwa kuabudu, kama wanavyoonekana baadhi yao wakiwa kiroho zaidi.

 Watu wakifunguliwa kwa njia ya maombi wakati Mwinjilisti John Sembatwa akiendelea kufanya maombi ya kufungua vifungo vya kubeba watu mioyoni kwa mabaya waliyotendewa.

 Ni maombi ya kushusha moto wa kimbingu.

 Watu wenye uhitaji mbali mbali wakiombewa.

 Watu wakiutafuta uso wa Bwana madhabahuni.

 Wahudumu wakiendelea kufanya maombi ya kufunguliwa kwa watu mbalimbali.

 Mtumishi Lukio Mjema (Aliyejishika uso) akimfanyia maombi mmoja wa watu waliofika kuombewa.

 Umati uliofurika kanisani hapo wakiwa wameshika sadaka zao mikononi wakiomba.

 Maombi ya kufunguliwa yakiendelea.

 Upande wa watu waliokaa ghorofani wakiendelea kushiriki ibada ya maombezi.

 Sehemu nyingine ya umati wa watu waliokaa ghorofani nao wakishiriki maombezi.

 Ndg. James akihakikisha watu waliokaa nje wanapata matukio yote na kumwona mhubiri live kupitia screen zilizowekwa kwenye mahema nje.

 Watu walifurika mpaka nje sehemu za parking ya magari. Hii inadhihirisha watu walivyo na kiu ya kumtafuta Mungu.

 Hawa nao walikosa nafasi ndani wakakaa nje. Pamoja na kuwepo jua kali lakini hawakujali.

 Wengine walikaa kwenye kibaraza cha jengo jirani na kanisa maarufu kama jengo la kitega uchumi.

 Mtumishi John akiwa ameshikilia kalenda ya mwaka 2016 kuashiria kuukabidhi mikononi mwa Mungu kupitia sadaka za mbegu walizotoa waumini.

 Wazazi wakiwa na watoto wao waliofika madhabahuni kuwaombea watoto wao ili wakue wakimjua Mungu.

 Sehemu ya watoto wakiombewa ulinzi wa Mungu uwe juu yao.

 Waumini wakiwa na watoto wao wakifuatilia maombezi

 Hivi ndivyo kulivyofurika umati wa watu wakifanyiwa maombezi, hakika Mungu alijifunua kwa watu hawa kwa njia mbalimbali.

 Kwaya kuu ya usharika wa Kijitonyama wakimtukuza Mungu kwa kuimba wakati wa ibada.

 Kwaya ya Vijana ya Usharika wa Kijitonyama wakiimba wakati wa ibada.

 Mwinjilisti Monyo akifanya maombezi wakati wa kuweka wakfu Photocopier machine, Laptop 1 na vitambaa vya madhabahuni vilivyotolewa kama sadaka na waumini wa usharika huo.

 Katibu wa baraza la wazee wa Usharika wa Kijitonyama, Bi. Victoria Kisyombe akitoa ufafanuzi kuhusu vifaa hivyo.

 Bi Victoria Kisyombe akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu vifaa hivyo na jinsi ambavyo vitafanyika msaada na kurahisisha kazi za usharika.

 Sehemu ya sadaka zilizotolewa jana katika ibada.

 Mzee Nikubuka Shimwela akibadilisha sadaka hiyo kuwa katika fedha ka njia ya mnada.

 Mzee Aminiel Mshana akitoa sadaka hiyo kwa Kwaya Kuu ya Usharikani hapo.

Mzee Aminiel Mshana akiinadi Kalenda ya mwaka 2016 iliyotengenezwa na Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.